Pages

Ads 468x60px

Friday, June 27, 2014

IMMANUELI MGOGO AWACHEFUA MAPRODUCER WA MKOA WA MBEYA,


WAMEDAI  AME WADHARAU NA KUWADHALILISHA  SANA, BITI ZA NYIMBO ZAKE AMETENGENEZA KATIKA STUDIO ZA MBEYA ADAI NI DAR-ES-SALAM
                               EMMANUELI MGOGO KATIKA ALBAM YA MSIKILIZE MUNGU
 NAMBA YA MAWASILIANO NA IMAIL YAKE VINAVYO ONESHA SI ALBAM  SI YA SAYUNI BAND BALI NA YAKE BINFSI
     TASWILA NDANI YA DVD YAKE INAVYO ONESHA VEDEO NA OUDIO  IMEREKODIWA WAPI 

KWA UNDANI WA HABARI HII SOMA HAPA CHINI


IMMANUELI MGOGO AWACHEFUA  MAPRODUCER WA MKOA WA MBEYA,

WAMEDAI  AME WADHARAU NA KUWADHALILISHA  SANA, BITI ZA NYIMBO ZAKE AMETENGENEZA KATIKA STUDIO ZA MBEYA ADAI NI DAR-ES-SALAM

Baadhi ya wamiliki wa studio  na waandaaji wa nyimbo za injili mkoani hapa wamemlalamikia mwambaji anae chipukia wa njimbo za injili EMMANUELI MGOGO kwa kitendo alicho kifanya cha  kuandika jina la Studio  ECK PRODUCTION ya jijini Dar-es-salaam  kwamba ndiyo iliyorekodi nyimbo zilizomo katika albam yake ya MSIKILIZE MUNGU wakati sikweli  nyimba hizo zimerekodiwakatika Studio za  hapa jijini Mbeya.

Hayo yamebainishwa na Produser wa Studio ya Braju Baraka Mwasambamba iliopo Airpot jijini hapa alipokua akiongea na mwandishi wa habari hizi, amekiita kitendo alichokifanya mwimbaji huyo si cha uungwana na hakina ustaarabu na hekima  ndani yake kwani ni kuudharau mkoa wa mbeya.

“Mwandishi kwanza ninasikitika sana kwa jinsi alivyo tudhalilisha Immanueli Mgogo  sisi waandaaji wa nyimbi mkoani hapa, mimi nimetengeneza Bit ya wimbo wa Msikilize Mungu, alikuja hapa na kwaya moja kwa lengo la kuwasaidia kurekodi  nilipotengeneza hiyo Biti kwa lengo la kuitengenezea hiyo kwaya yeye akasema naomba usiwape hawa ninaitaka niitungie maneno nikamkubalia” alibainisha Mwasambamba

Ameongeza kua baadae alikuja na kuaanza kuingiza maneno tukiwa wote hapa Studioni kwangu, tulipo maliza aliniomba aichukue data apelike Dar es salaam ampelekee mpiga kinanda amjazie maeneo yaliyo acha wazi mimi nilikubali nikampa hizo data nashangaa sana kuona ndani ya hiyo DVD  yake ameandika OUDIO imetengenezwa na ECK  PRODUCTION huu ni udhalilishaji.

Baraka amehoji kwamba kama kweli nyimbo hizo zomerekodiwa Dar es salaama anaweza kudhibitisha?, je wale waimbaji wanao mwitikia alikwenda nao huko ECK? Alihoji huku akiwa na jazba kwa jinsi alivyolipokea swala hilo, tunajua waimbaji wengi wa huku Mbeya wakiisha pata majini kidogo tu  hupenda kuhamia huko lakini si kututukana matusi watu wa mkoa huu kama huyu.

Kwa upande wake Producer  Peter Mbuba wa H Studio iyopo maeneo ya Isanga jijini hapa yeye kasema anamuachia Mungu kwa kitendo alichokifanyiwa na mwimbaji huyo kwani amesikitishwa sana baada ya kuona wimbo alioutunga Producer huyo na kuutengenezea Bit yake  anakuta anatukuzwa mtu mwingine.

“Mimi ndiye niliyetengeneza biti na maneno ya wimbo wa Niko ulieko nimeiga kutoka kwa mwimbaji wa Afrika kusini Rebeka Marope nashangaa leo hii naona katika cd yake kwamba imetengenezwa Dar es salaam na Studio ya ECK hii si sawa hata kama ameona Mbeya hakuna watengezaji bola angetengeneza huko”

Bwana, Mbuba ameongeza kwamba hata kama Mgogo atapinga haya yeye anao ushahidi wa nyimbo hizo ikiwa ni pamoja na biti za kinanda chake hakiingiliani na vinanda vingine anaweza kutoa ili kilinganishwe na huyo anaemwita ECK, wa Da es salaam  kwamba ndiye alie recod nyimbo hizo, kwakufanya hivyo ni sawa na kuukataa mkoa wake ulio mtoa.

Nao baadhi ya waimbaji aliokua akiimba nao katika albam ya kwanza iliyokua ikiitwa Iko wapi njia ya Sayuni Band kwa kutotaka kutajwa majina wamesema wao katika albam ya Msikilize mungu hawajahusishwa na kwamba hawajui imerecodiwa lini wapi na kwa gharama gani na hata mapato yake hatuyajui.

“Ukweli ni kwamba Mgogo katika Sayun bandi ni mwalimu tu na atabaki kua mwalimu sisi albam ya Msikilize mungu Hatujashilikiswa kwa hiyo si ya Sayuni Bandi hiyo ni yake kama mgogo na ndio mana ukiangali  Imeandikwa Immanueli mgaga hilo neon Sayun Bandi ameliweka tu wala si Sayuni Badi” Hyo yamesemwa na baadhi ya waimbaji wa Sayuni Bandi.

Awali mwambaji Immanueli mgogo amekua akijipatia umaarufu katika uimbaji wa nyimbo za injili ambapo mwanzoni mwa safari yake ya uimbaji ilianzaia katika Albam ya kwanza iliyoitwa Iko wapi njia iliyo kua chini ya Sayuni Band, albam hii ilitokea kutamba sana katika vymbo vya habari na hata katika matamasha mbalimbali, na kitu ambacho kimemfanya  atambulike ndani na nje ya mkoa wa Mbeya

Kama ilivyo kawaida ya baadhi ya watu wanapo pata nafasi ya kupata umaarufu kidogo husahau aliko toka na kujiona mafanikio hayo yamekuja kwa nguvu na juhudi za akili zake na kusahau msemo wa wahenge uliokua ukisema ukimuona kobe juu ya mti ujue kapandishwa.

0 comments:

Post a Comment