Pages

Ads 468x60px

Friday, June 6, 2014

TOPSy KRETTS: Toleo Na. 4 FREEMASONRY



FREEMASONRY
Freemasonry inaweza kutafsiriwa kwa namna mbalimbali  lakini … is fraternal organizational whose members, help each other and communicate using secret signs.

Kwa maana hii kwamba “Freemasonry”… ni jumuiya ya watu wenye nia ya kusaidiana kila mmoja, ambao huwasiliana kwa kutumia alama za siri.
Hakuna mwanadamu aliyezaliwa kuwa freemasonry ila ni matakwa binafsi ambayo binadamu huyu anataka katika maisha yake, hasa ikizingatiwa kuwa binadamu ameumbwa na mwili, nafsi na roho.
Hivyo, kila kimoja katika hivyo hutafuta matakwa yake binafsi ili kukamilisha haja yake na ni uamuzi wa binadamu huyu kuamua ni njia ipi ya kwenda katika maisha yake ya kila siku.
Asili ya Freemasonry
Asili ya kundi hili imetoka mbali sana hata kuja kuitwa Freemasonry. Ukiisoma katika Biblia kwenye vitabu vya Injili kuna mahali Yesu wakati wa huduma yake ulimwenguni alizungumza kuhusu “Kizazi cha Nyoka”- (Brood of Vipers).
Msomaji jiulize swali hili ilikuwaje mpaka akatamka maneno hayo magumu?...
Historia Fupi ya Kizazi cha Nyoka
Kizazi cha Nyoka kilitanuka zaidi kutoka Mashariki ya Kati, Asia, Ulaya na Amerika. Na hii ndio sababu ya kuona jambo hili ni gumu barani Afrika lakini kwenye maeneo tajwa ni suala la kawaida.
Ili kujua kwa undani zaidi kuhusu FREEMASONS ni lazima ujue kwanza Historia ya Kale na Utamaduni.
Historia ya Kale hadi Freemasons
Wamisri wanasema miungu au waungu wao waliojulikana kama wachawi walikuja na boti zinazolea angani. Hii ni kwa ufupi tu kwa habari ya maendeleo ya watu wa kale, ya watu wa Mesopotamia.
Jamii ni nyingi duniani zinaelezea kuhusu uvamizi wa kabila hilo jipya, au miungu ilivyokuja kwao na aina ya vyombo vieleacyo angani, na kuingiza maarifa, pamoja na ustaarabu mkubwa katika jamii.leo hi vyombo hivyo vinajulikana kama UFO yaani Unidentified Flying Object.
Na taarifa za Serikali ya Marekani na nchi nyingine za Ulaya zinasema hakuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha madai hayo yahusuyo jamii za kale na wageni kutoka nje ya dunia.
Lakini mbona taarifa hizo hazisemi chcochote kuhusu kile kilichotokana na wageni hao? Ustaarabu wa hali ya juu, ujenzi wa ajabu ambao hata leo, pamoja na teknolojia iliyopo, itatugharimu mengi kuufanikisha ujuzi huo wa watu wa kale.
Mbona taarifa zilizopo hazisemi lolote kuhusu elimu ya sayari zilzopo na mifumo yake ya jua, ambayo ndiyo kwanza vinagunduliwa sasa na wanasayansi wetu vikiwa vinafanana kabisa na vile vinavyoelezwa na wageni hao maelfu ya miaka ya nyuma kabla ya Kristo?.
PREVIOUS CHAMBER

0 comments:

Post a Comment