Kaimu mkurugenzi wa kampuni ya Seed co nyanda za juu kusini Michael Rikanga akiongea na waandishi wa habari na kuonesha mbegu wanazotegemea kuingiza katika kilimo msimu huu
Waandishi wa habari mkoa wa mbeya wakimsikiliza kwa makini Rikanga
Hii ndiyo form maalimu ya kujisajili katika shindano hilo
Shule ya msingi Nsoho iliyopo nje ya jiji la mbeya ambapo mwandishi wa habari hizi alifika kupata maoni ya waalimu na wanafuzi wanapokeaje shindano hili
Baadhi ya mashamba ya shule hiyo yaliyokodishwa kwa wanakijiji yakiandaliwa tayali kwa kilimo kwa msimu huu wa kilimo
Msitu uliopandwa kuizunguka shule hiyo kama mradi ambao inasemekana umesababisha kukausha mto uliokua kipita na kutililisha maji karibu na shule hiyo
Baadhi ya makazi ya wanakijiji wa Nsoho wanaoizunguka shule hiyo
Mwandishi wa habari hii akipita katika bonde lilikauka maji na akishuhudia kutoweka kwa mto uliokua ukitililisha maji kwa msimu wote ukiwa umekauka
HABARI KAMILI
Kampuni ya
pembejeo Tanzania Seed co LTD imezindua rasmi shindano la shama darasa katika
shule za msingi, ambapo shule itakayokua imelima shamaba zuri kwa kuzingatia
misingi yote ya kilimo bora cha kisasa itajishindia zawadi kubwa ya madawati
miamoja yenye thamani ya milioni kimi na tano.
Akiongea
katika mkutano na waandishi wahabari uliofanyika katika ukumbiwa mtenda jijini Mbeya
MICHAEL RIKANGA kaimu mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema lengo la shindano hilo
ni kutaka kuisaidia jamii na kuiunga mkono serikal kauli mbiu yake kua uti wa
mgongo wa Tanzania ni kilimo.
“Tumeona ni
vema tuhamasishe kilimo bora huku chini kabisa katika shule za msingi kwakua kumekua
na elimu mbalimblia zinazo pita kwa jamii ambayo haziwagusi wananchi wa chini hivyo
kama kampuni imeamua kuanzisha shindano hili kwa shule za msingi ili
wanapomaliza kidato cha nne wawe na uelewa wa kilimo kwakua wengi hurudi kuwa
saidia wazazi kazi za kilimo” amesema Rikanga
Ameongeza
kua pamoja na vijana waliopo vijijini kuendelea na shughuli za kilimo basi ni
viema wakajifunza kilimo bora na cha
kisasa ambacho watakua wamejinifunza katika mashamaba darasa yaliyopo mashuleni,
Hivyo kukuza kilimo cha Tanzania kwa kutumia pembejeo zilizo bora na kuongeza
kipata kwa jamii
Katika
mkutano huo Rikanga ametambulisha mbegu mpya aina ya chapa tembo yenye ubora
mkubwana ambayo katika hekali moja ukilima kwa kufuata kilimo cha kisasa
mkulima anauwezo wa kuvuna zaidi ya magunia albaini na amewataka wananchi
kuzitumia mbegu hizo ambazo zimefanyiwa utafiti na maraka husika.
Kwa upande
wa mwalimu wa shule ya msingi Nsoho
Rugano kajisi iliyopo nje ya jiji la Mbeya amesema shindano hilo ni zuri na
wanalipokea kwa moyo mkubwa japo habari hizi hawajazipata na wala hawajui kama
kunashindano la aina hiyo lakini wakipata nafasi ya kushiliki watajitahi
kufanya vizuri kwani zawadi ya madawadi 100 yataisaidia shule yao.
“Ukweli ni
kwamba sisi kama shule ya msingi Nsoho hatujasikia kama kuna shindano la aina
hiyo endapo tukipata nafasi ya kushiriki tutajitahi kufanya vizuri na
kujishindia hayo madawati 100 kwa kua mashamba tunayo lakini hatuyalimi zaidi
tunawakodishaia wanakijiji tukiingia katika shindano hilo tutayalima sisi
wenyewe” amesema Kajisi
Ameongeza
kua shule haina miradi ya kuingizia kipato kikubwa endapo watapata elimu ya
kilimo cha kisasa itawasaidia kuanzisha mradi wa kilimo na kuisaidia shule
kuongeza kipato, kwani mpaka sasa wanategemea miti iliyo pandwa kizunguka shule
hiyo kama mradi wa kuwapatia kipato.
Pamoja na
kuwa na mradi hua bado ameulaumu kwakua miti iliyo panda imekua ikinyonya maji
kwa wingi ambapo inaweza kusababisha ukame kwani mpaka sasa chini ya shule hiyo
kuna mto wa maji ulikua ukitililisha maji kwa mda wote kwa sasa umekauka
kutokana na msitu uliopandwa karibu yake.
Kwa upande
wa wanafunzi wa shule hiyo walipta nafasi ya kuhojiwa na mwandishi wa habari
hizi wamefurahishwa sana na shindano hilo na kuahidi kushiriki kwa nguvu zote
ili kujinyakulia zawadi hiyo kwani wamekua na uhaba mkubwa wa madwati katika
shule yao hivyo hiyo wanaiona ni fulsa ya kujikwamua na tatizo la muda mlefu.
Shindano
hilo litaanza haraka iwezekanavyo katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2041-2015
na kwa habari zaidi za shindano hili zinapatika katika gazeti la nipashe.
0 comments:
Post a Comment