Pages

Ads 468x60px

Monday, October 27, 2014

Timu ya Mbeya city mambo yanazidi kuwaendea kombo Yachezea kichapo na Mtibwa suger,



Mashabiki wamtaka Kocha wa timu hiyo Juma mwambusi kujiuzuru.
 Kocha Mbeya city Juma mwambusi akiongea na vyombo vya habari (Picha na maktaba yetu)

              Timu zote mbili zikiingia uwanjani kisha kukaguliwa nakuanza mtanange



                                    Kila timu zikifanya Dua kwaimani yake






                                      Mashabiki waliojitokeza kushangilia timu yao

















                        Tazama katika habari picha jinsi mchezo huo ulivyo kwenda
Baada ya kufungwa gori la pili mashabiki wakaanza kurusha mawe na makopo ya maji uwanjani

              Baadhi ya wachezaji na mashabiki wakitoka uwanjani wakilia machozi


                                                           Habari soma hapa
Na, Charles Abraham


Timu ya Mbeya city mambo yanazidi kuwaendea kombo Yachezea kichapo na Mtibwa suger,
Mashabiki wamtaka Kocha wa timu hiyo Juma mwambusi kujiuzuru.

Ni siku chache zimepita tangu timu ya Mbeya city iendeleze uteja kwa wana lambalamba Azam fc wa jijini dare s slaam kwa kuchapwa gori 1-0 na kuwatia machungu mashabiki wake ambao msimu uliopita walikua wakisherehekea raha za ushidi.

Jana tena timu hiyo imeendelea kuwanyima raha mashabiki hao kwa kuchezea kiminyo cha bila huruma 2-0 kutoka kwa wakata miwa Mtibwa Suger ya mjini Morogoro na kuwafanya wacharuke na kurusha mawe ndani ya uwanja baada ya kupachikwa bao la pili.
Mashabiki hao wakiongea kwa nyakati tofauti wamemtaka kocha wa timu hiyo Juma mwambusi kuchukua hatua ya kujiuzuru kutokana na kuwa yeye ndiye chanzo cha matokeo na mwenendo mbovu wa timu yao.

Akiongea moja wa mashabiki hao Razalo Mgwenda huku akitokwa machozi ameutaka uongozi kuchukua hatua za makusudi haraka iwezekanivyo kuongea na wachezaji kujua nini tatizo ili kuinusuru timu hiyo kabla haijafikia pabaya zaidi.

“Mimi nimechoshwa na kila wikiendi kuumizwa kichwa kwa kuja kushangilia timu yangu lakina haifanyi vizuri kila siku inafungwa kuanzia leo siji tena huku siko tayali kukosa raha kwani timu yenyewe haitupi hata nafuu ni kutuumiza tu” amesema shabiki huyo.

Pamoja na hayo kumekua na tetesi kutoka wadau hao wakiendelea kumtupia lawama Juma mwambusi kwa kuwapanga wacheza kwa manufaa yake binafsi, wamesema kuwa endapo mchezaji hakumpatia asilimia fulani ya posha yake hawezi kupewa nafasi ya kucheza.

Katika malalamiko hayo inasemekana wachezaji wenye uwezo hawakubaliani na hilo hivyo hawampatii posha hiyo kwa kuringia uwezo walionao na ndipo hawapangwi na ikitokea kacheza basi ni hucheza dakika chache za mwisho wa mchezo.

Kwa upande wake kocha huyo ameyapokea matokeo hayo kwani amekiri na kuona umuhimu wa kukaa na wachezaji wake ili kuangalia ni nini kilicho wapata msimu huu kwa kua hii ni mchezo wa pili wanapoteza wakiwa kiwanja cha nyumbani.

“ Nikweli nimepokea matokeo haya kwauchungu sana kuna haja kubwa kukaa na wachezaji wangu kuangali nini kimetokea kwakuwa hii ni mechi ya pili tunapoteza tukiwa nyumbani kitu ambacho hakijazoeleka Tutakaa chini Tujipange tuone cha kufanya” Amesma mwambusi

Nae kocha wa Mtibwa Suger Mecky mexime amekiri kuwa mechi anazo kutana nazo ni ngumu lakini wamejipanga vizuri amewasifia wachezaji wake kuwa wana hali ya kushinda nakwamba nafasi waliyopata wamezitumia vizuri  na ndio maana  wamepata matokeo hayo.

                                                                             MWISHO




   

0 comments:

Post a Comment