Wazee
wanyanyaswa na kunyang`anywa milki zao huko matema wilayani Kyela
Mbeya Moraviani Town choir watembelea na kujionea kisha kuwapatia misaada mbalimbali
Waimbaji wa nyimbo za injili mkoni mbeya Town choir wakiwa na wenyeji wao tayali kwa kuwatembelea wazee
Bibi amelala chini ishara ya kushukuru baada ya kupewa zawadi na wanakwaya hao, Bibi huyu ameachwa na wajukuu wanne na watoto wake waliofariki wakiwa wanantegemea na hana kipato chochote
Vijana hao wakiondoka kwenda kaya nyingine
Bibi huyu hana ndugu yoyote wakumsaidia na hiyo ndiyo nyumba yeke amejengewa na wasamalia wema haina choo wa jiko na maisha yanaendelea kijana mmoja yohana kajange amejitolea bati ili kuezeka ama kujenga upya nymba hiyo.
Baadhi ya waimbaji watokwa na machozi walishindwa kuvumilia waliyokua wakiyaona jinsi wazee hawa wanavyopata tabu katika maisha yao
Ziara inaendelea
Bibi huyu ana mtoto mmjoa lakini amemtelekeza kwamba amewahi mtukana hivyo hampi msada wowote na anasumbuliwa na kifua kikuu hivyo anahudumiwa na wasamalia wema.
Hiyo ni nyumba ya bibi hawa wawili ni mtu na mdogo wake wamefukuzwa kutoka katika miji ya waume zao baada ya kufa hivyo wamerudi nyumbani kwao na kujengeawa kibanda hicho ambacho hujihifadhi.
Hii ni nyumba ya bibi huyo hapo juu ambae tulimkuta amelala chini ya kivuli cha mti akiwa hana mtu wa kumsaidia
Huyu anaumwa kavimba miguu na hana mtu wa kumtuma amletee hata maji ya kunywa
Ziara bado inaendelea
Zaidi ya kaya 25 zilipewa msaada na waimbaji hao
Baada a ziara mambo kunoga
Ziara ya siku mbili sasa ni wakati wa maandalizi ya kulejea jijini
Soma habari hapa
Ukatili wa kijinsia bado ni tatizo
kubwa nchini Tanzania
Wazee wanyanyaswa na kunyang`anywa
milki zao huko matema wilayani Kyela
Pamoja na
mashirika malimbali yesiyo ya kiserikali nchini yanayo pinga na kutoa elimu ya
unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hari hiyo bado ni kitendawili katika jamii
ya watanzania.
Hali hiyo
imegundulika baada ya kikundi maarufu cha uimbaji wa nyimbo za Injili Nchini
Mbeya moraviani town choir cha kanisa la moraviani ushirika wa mbaeya mjini
kufanya ziara huko matema.
Kikundi hicho
kimefanya ziara ya kuwatembelea wazee wanaoishi mazingira magumu katika kijiji
cha matema kilichopo wilayani Kyela na kukuta hali hiyo inayo pelekea majonzi
mazito.
Akiongea
mwenyeji wao Mchungaji Zabroni Mwakalasi wa kanisa la (KKKT) matema amesema wazee
hao wametelekezwa na familia zao, na wengine kutokana na mila za eneo hilo zime
wafanya wajikute wametengwa bila msada wowote
“Hawa wazee
wameachwa na familia zao kwa imani tofauti ikiwepo kufukuzwa katika miji yao
baada ya mume kufa ndugu wanaobaki huwafukuza ili kumiliki mazao yaliyopo
katika mashamba hayo likiwepo zao la kokoa ambalo limeku na kipato kikubwa kwa
jamii ya watu wa kyela” amesema mwakalasi
Kwa upande
wao mmoja wa wazee hao amewashukuru sana Vijana hao kwa moyo waliouonesha kwao
kwani yeye amekata tama ya kuishi kwa kudhani hana ndugu wakumfariji
“Asanteni
sana kwa kututembelea sisi wazee ninamshukuru Mungu aliewaleta kwetu kwani
tulidhani hatuna ndugu tena kumbe tunao tena ni wengi katika kristo yesu”
aliongea huku akitokwa na machozi ya uchungu.
Vijana wa
Kanisa la moraviani ushirika wa Mbeya mjini walifanya ziara hiyo ya siku mbili mwishoni mwa
wiki hii katika fukwe za ziwa nyasa (matema) kwa lengo la kupanga mpango
mkakati wa maendeleo yao kwa mwaka 2014-2015
Katika ziara
hiyo pia walipata nafasi ya kutembelea wazee wanaoishi mazingira magumu ambapo
walitoa misaada mbalimbali ikiwepo Sukari, chumv, sabuni, mafuta ya kupakaa na
box la viberit.
Kiongozi wa
ziara hiyo John mwambola ametoa wito kwa vikundi vingine na watu binafsi
kutembelea watu wenye uhitaji kama hawa kwani wanahitaji sana faraja na misada ya hali na mali kwa mazingira waliyojikuta
wakiiishi bla kupanga.
Mwambola maongeza kua kwakufanya hivyo ni kutimia amri kuu tuliyo achiwa na bwana wetu yesu kristo alipokua akiondoka hapa duniani yani (UPENDO)
0 comments:
Post a Comment