Mkuu a wilaya ya Mbeya Norman Sigalla akiongea na viongozi wa dini na siasa
Viongozi wa Dini, Siasa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya mbeya
Wadau wakichangi maoni katika mkutano huo
Habari kamili
Viongozi wa dini na vyama vya siasi
wametakiwa kuilinda amani mkoani Mbeya
Kwakua Mbeya ilikuwepo kabla ya
taasisi hizo
Hayo yame
jili katika mkutano wa viongozi wa dini, siasa na kamati ya ulinzi na
usalama wilaya ya Mbeya mjini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
halmashauri hiyo jijin hapa
Akiongea
katika kikao hicho mkuu wa wilaya ya Mbeya Norman sigalla amewataka viongozi hao kuchukua hatua ya kuilinda amani ya wilaya
na mkoa kwa ujumla kwakua Mbeya ilikuwepo kabla
ya taasisi hizo kuwepo.
“Ndugu zangu
nawaomba kuilinda amani ya wilaya kwa dhati kwakua dini na siasa si muhimu
kuliko Mbeya yetu, kwakua ipo kabla hata ya dini na vyama vya siasa kwa hiyo ni
muhimu kuendesha dini na siasa kwa uangalifu mkubwa ili kusitokee kuihatalisha
amani yetu” amesema Sigalla
Ameongeza
kua machafuko ya dini yanatokea sana huku Afrika, lakini ziliko anzia dini hizo
hawagombani huwezi kuona Uarabuni au Ulaya watu wanagombana kuhusu dini yao
jiulize ni kwanini waanzilishi hawapigani ila wapokeaji hupigana ujue ipo shida katika
uelewa wao.
Pia Sigalla
amewataka viongozi hao kujiuliza kitu chochote wanacho kifanya kina manufaa
gani kwa jamii ya watanzania na kinalaeta maendeleo gani kwao ukiona unapamga
maandamano unaona kabisa hayana umuhimu kwa maendeleo yao ni bora sana
ukayaacha.
Kwa upanda
wake makamu wa Shekhe wa mkoa Abdull Azizi amewataka vingozi wote kuchunga sana
ulimi kwakua ndicho chanzo kikubwa cha mafarakano mahali popote duniani kwani
huchochea na kusababisha machafuko, hata hinyo amempongeza mkuu wa wilaya hiyo
kwa kuwa na utaratibu wa kukutana nao mara kwa mara.
Kwa upande
wa mmoja viongozi wa siasa Yasini mlotwa
mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) wilaya ya mbeya ameishauri serikali kuchunguza tenda
zinatolewa huchukuliwa na mawakala feki wengine wakiwa watumishi wa serikari ambao
hushinda na kufuja pesa za walipa kodi bila manufaa yao.
Mkutano huo
ni mkakati wa mkuu wa wilaya ya Mbeya na wadau hao waliojiwekea ili kukutana kila baada ya miezi
sita kwa lengo la kutathimini muenendo wa amani katika wilaya na mkoa wa Mbeya.
0 comments:
Post a Comment