Pages

Ads 468x60px

Tuesday, October 21, 2014

Maka Mwalwisi ndie mchawi wa Mbeya city?

Matukio katika picha mchezo wa mbeya city na Azam fc






















                                      Wachezaji wa timu ya Azam fc wakishangilia goli


                                                            Ulinzi ukiwa umeimalishwa













                                  Mashabiki mbeya city wakilia baada timu ao kufungwa


                                     Mashabiki wakiongea kwa uchungu baada ya timu yao kufungwa

                                                                            Habari kamili



Maka Mwalwisi ndie mchawi wa Mbeya city?
Mashabiki wamtafuta mchawi, kwani hali si shwali msimu huu kwao
Yachezea kichapo na wana lambalamba Azam fc kiwanja cha nyumbani

Katika hali isiyo ya kawaida msimu huu Timu ya Mbeya city iliyo tamba sana msimu uliopita kwa msemo usemao ukiingia hutoki hali hiyo imegeuka na kua ukiingia upetupata baada ya michezo yate iliyocheza katika uwanja wanyumbani haijaonesha makali yake.

Timu hiyo ilipandaraja msimu uliopita na kuonesha kiwango cha juu sana chenye ushundani na kumaliza msimu huo kwa kushika nafasi ya tatu ikiongozwa wanalambalamba hao ambao wameendelea kuwanyima raha Mbeya city wakiwa katika kiwanja cha nyumbani

Mbeya city wamekwisha cheza michezo minne wame droo michezo miwili, wameshinda mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmjoa kati yake na Azam fc kwa kichapo cha 1-0 na kuifanya timu hiyo kushindwa kutamba kwa mala nyingine tena ikiwa nyumbani.

Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wamekua na maoni mbalimbli ikiwepo kuhoji kwamba mwanzo huo usio wa kulidhisha kumesababishwa na aliekua mwalimu namba mbili Maka mwalwisi ambae hakusaini mkataba msimu huu na kutimkia Panoni ya Moshi,Ambako amenyakua nafasi ya kua kocha mkuu wa timu hiyo

Kwa matokeo hayo baadhai ya mashabiki walitoka uwanjani hapo wakiwa wameinamisha nyuso zao chini huku wengine wakitokwa na machozi kuashilia kuumia kwa mwenendo wa timu yao na kusababisha utulivu mkubwa katika jiji la Mbeya mabalo huzizima timu hio wanapopata ushindi.
Kwa upande wa kocha wa timu hiyo Juma mwambusi amesema katika mchezo wowote kuna matokeo matatu kushinda, kutoa sale na kufungwa, kati ya hayo wanakubaliana na matokeo lakini wanajipanga vizuri michezo ijayo.

                                                        MWISHO

0 comments:

Post a Comment