Pages

Ads 468x60px

Thursday, March 19, 2015

Malaka ya maji safi na maji taka jijini Mbeya kuzindua chemba ya maji taka katika shule ya Sekondali Rejiko



Wakati tukio hilo likijili wananchi wakata ya majengo wakusudia kuiburuza mahakamani malaka hiyo kwa kushindwa kudhibiti chema hizo zinazotililisha majitaka hovyo mitaani na kuhatalisha afya zao.

 Shimo la chemba likijengwa kwa haraka na mafundi ili kuzinduliwa hiyo kesho na malaka ya maji taka katika shule ya sekondali Rejiko

Baadhi ya afisa wa maji taka akiwepo mkuu wa shule mwenye shati la bluu na msimamizi wa kitengo cha maji taka Tumaini kalala alieweka mkono mfukoni wakisimamia ujenzi wa chemba hiyo.



 Mita chache toka hapo nichemba ya maji taka ilikua ni kelo ya zaidi ya mwaka mmoja na inayotililisha maji yake katika mto dauseni unaotumiwa na wanafunzi pamoja na wakazi wa eneo hilo kwa matumizi mbalimbli ya kijamii.



 Chemba hiyo inatililisha majitaka katika mto huu na wanafunzi wa shule ya sekondali Rejiko wanachota maji yake kwa matumizi mbalimbali shuleni hapo.
 Afisa mtendaji kata ya Majengo Charles mwandembwa akiongea na mwandshi wa habari hii ofisini kwake.

Soma hapa:



Malaka ya maji safi na maji taka jijini Mbeya kuzindua chemba ya maji taka katika shule ya Sekondali Rejiko

Wakati tukio hilo likijili wananchi wakata ya majengo wakikusudia kuibuluza mahakamani malaka hiyo kwa kushindwa kudhibiti chema hizo zinazotililisha majitaka hovyo mitaani na kuhatalisha afya zao

Katika hali  hiyo ya sintofahamu iliyowakumba wakazi wa kata ya Majengo jijini hapa wameshangazwa  na hatua ya Mamlaka hiyo kupanga kuifanyia uzinduzi chemba   mpya ya maji taka huku wakiwa na kilio cha muda mlefu cha kutengenezewa chemba inayotililisha maijitaka  kwa muda mlefu na kuhatalisha afya zao  bila mafanikio.

Wakiongea kwa nyakati tofauti na kwa masikitiko mkubwa wakazi wa kata hiyo, mkazi wa kata aliyejulikana kwa jina la mama Dony amesema kua mamlaka hiyo haijajipanga vizuri katika kutekeleza  mradi huo kutokana na kutokua makini katika kutatua kwa haraka changamoto zinazotokana na mradi huo.

“Niasikitishwa zana na wahusika wa mradi huu sisi kama wakazi wa majengo tumekua tukilalamika sana juu ya maji haya yanayotoka katika chemba hiyo na kuingia katika mto huu ambo maji yake watu wanatumia katika shughuri mbalimbali ikiwemo kufua na kufanyia usafi majumbani tumekwenda kwa balozi, Afisa mtendaji hata diwani wote wameshindwa kutusaidia kutatua shida hii” amesema mama Dony

Nae RiCHARD MWAMBONA amesema kua  kutokana na juhudi za kila namna kugonga mwamba wao kama wakazi wa majengo wanakusudia kuibuluza mahakamani malaka hiyo kwani ina lengo la kuwaletea mlipuko wa magonjwa kwa wakazi hao ikiwemo maralia na kipindupindu.

Kwa upande wake SHUMBA HARIFA balozi wa mtaa huo ameseama chemba hiyo imekua kelo kubwa sana ya mda mlefu  kwa wakazi wa mtaa huo, Na kuongeza kua wamepeleka mala kadhaa malalamiko hayo kwa malaka ya  maji taka lakini wamekua wakiwaambia kwamba hawana vifaa na wameviagiza nje ya nchi wakti huo huo mamlaka hiyo inataka kufanya uzinduzi wa chemba  na kuaacha kushughurikia matatizo kama yao.

Juhudi za kumpata msemaji wa malaka hiyo ziligonga mwamba kutoka na kurushiana mpira baada ya kuonana na  mhusika anaeshughulikia mitalo  hiyo aliejulikana kwa jina moja la GODFREY na kusema yeye si mseamji bali ni TUMAINI KALALA ndiye msimamizi wa kitengo cha maji taka naye  ilikana na kusema yupo msemaji ambaye alimtaja kwajina la Ing:  PAULO MLOELYA ambae ni mkuu wa kitengo cha maji taka tulimtafuta katika simu yake ya kiganjani hakupatikana.

Afisa mtendaji wa kata hiyo CHARLES MWANDEMBWA amekili kuwepo kwa tatizo hilio na malalamiko  mengi kwa wakazi wa eneo hilo lililodumu kwa muda mrefu sasa  na kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo lakini hakuna mafanikio yoyote mapaka sasa.

MWISHO.





0 comments:

Post a Comment