MWENEKITI WA BODABODA MKOA WA MBEYA VICENT MWASHOMA AKITOA TAMKO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI NA VIONGOZI WA VITUO MBALIMBALI KATIKA UKUMBI WA COFE GARDEN
KATIBU MSUMBS MDESA AKISOMA TAMKO MBEYA YA WANACHAMA NA WAANDISHI WA HABARI
BAADHI YA VIONGOZI WA BODABODA WAKIWASIKILIZA VIONGOZI WAO
UJUMBE WAO KUPITA MABANGO WAKIONESHA KWA WAANDISHI WA HABARI
Soma hapa
Na Charles Abraham:
Viongozi wa chama cha bodaboda mkoani
Mbeya wagomea zoezi la kubadili namba mpya.
Wadai kodi yake ni kubwa na ni mzigo
mzito kwao hawana uwezo wa kuubeba
Chama cha bodaboda mkoani Mbeya wametoa tamko la kuto
endelea kulipa kodi za kubadili namba mpya linalo tegea kumalizika mach 31/
2015 kwa mujibu wa mamraka ya mapato Tanzania (TRA) na kwamba endapo
hawatabadili kwa muda huo basi watalipa gharama hizo pamoja na faini
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
ulifanyika katika ukumbi wa cofi garden uliopo jijini hapa mwenyekiti wa chama
hicho VICENT MWASHOMA amesema hawawezi kutoa gharama hizo kwakua serikali
haijatoa elimu vizuri kwa waendesha bodaboda kwani ni tofauti na ukienda kulipia
“Ndugu waandishi Serikali
ilikua na dhamila nzuri katika kuendesha zoezi hili la kubadilisha
kutoka namba za vibao vya njano kwenda vyeupe hii ingerahisisha usimamizi na
utawala kwa pikipiki zetu lakini pia kuzipata zilizoibiwa hii ilikua ni nia
njema, Tuliambiwa tutalipa shilingi elfu kumi tu, sasa ni tofauti na ukienda
kulipa tunalipishwa kiasi cha laki moja
hadi laki tano kitu ambacho hatuwezi kumudu” amesema Mwashona
Kwa upande wake katibu wa chama hicho MSUMBA MDESA amesema
kuanzia leo wamesitisha zoezi la usajili wa namba mpya za pikipiki kwa kuiambia Serikali hawapo tayali kwa
utaratibu waliouanzisha wa ulipishwaji wa gharama za usajili wa vyombo vyetu
kwakua tunajua tunaonewa .
“Nataka kusema kuanzia sasa hatutalipa gharama hizo ili
kulipia namba mpya kwakuwa kwani anaepaswa kulipa ni muuza duka anapo ingiza
chombo nchini anatakiwa atozwe hiyo kodi ya lakini si mtumiaji wa mwisho ambae ni
kijana wa kitanzania aliyekosa ajira na kuchukua mkopo ili kujiajiri iSerikali
inakuja kumkandamiza kwa kumtwisha mzigo mzito wa kodi kubwa hata kabla ajaanza
kurejesha mkopo. Amesema Mdesa.
Ameongeza kuwa anaiomba serikali iliangalie upya swala hili
na kutengeza mazingira mazuri kwa vijana
wanaotafuta namna ya kujiajiri
wasiweke mazingira ya kutaka tuandamane.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment