Imeelezwa kuwa wilaya
ya Chunya ina rasilimali nyingi ambazo
zinaweza kuwaondoa wananchi wake kwenye umaskini pia kuifanya wilaya hiyo kuwa tajiri na kuwa nufaisha wananchi wake.
Hayo yamebainishwa na
HARUNA MWANAUTA ambaye ni mfanya
biashara mkubwa katika sekta ya utarii na uwindaji wa wanyama poli katika kitalu cha Rungwa
mwamagembe kilichopo Lupa wilayani humo.
Mwanauta ameyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari
kuwa wilaya hiyo inayo dhahabu nyingi na
wachimbaji wakubwa ambao wanaweza kuinufisha kwa kodi zao na pia kuwaunganisha
wachimbaji wadogo ili waweze kukopesheka na kununua vifaa vya kuchimbia
HARUNA MWANAUTA |
Amesema swala la wilaya hiyo pamoja na wananchi wake kuitwa masikini yeye anapingana nalo, nakumesema kuwa nikuwakosea wananchi wake kwani wanayo migodi ya Dahabu pamoja na kilimo cha Tumbaku ambacho kinaweza kuwa kwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini uliokithili .
“Chunya inahitaji
kiongozi mwenye ushirikiano na wananchi
katika kuwajengea uwezo wa kujikwamua katika umasikini uliopo , Kwani
imegawanyika katika makundi mawili makuu kiuchumi ikiwepo Dhahabu na kilimo cha
Tumbaku lazima apatikane kiongozi atakae wezesha sekta hizi mbili ziwanufaishe
wananchi wa chunya” amesema Mwanauta.
chunya ina ardhi yenye Rutuba inayo kubali kilimo cha aina yoyote, wananchi waatumie maafisa ugani kulima kilimo chenye tija na kutumia fursa ya uwanja wa Ndege wa songwe kuuza nje ya nchi mazao yao
Aidha mwanauta amekua akiiangalia wilaya hiyo kwa
mtazamo wakipekee na kuona fursa iliyo nayo ya dhahabu pamoja na kilimo
kinaweza kuwanufaisha kisha kuondokana
dhana iliyo jengeka kwamba wilaya hiyo ni masikini pamoja na wakazi wake, ameamua
kujitosa kugombe nafasi ya ubunge
muda utakapofika na kumrithi Victor Mwambalaswa aliyepo sasa
0 comments:
Post a Comment