Pages

Ads 468x60px

Monday, April 20, 2015

Nyalandu amaliza mgogoro Mbarali



WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu karibu miaka 10 wilayani Mbarali, mkoani Mbeya.
Mgogoro huo unahusisha wakazi wa vijiji 21 waliotakiwa kuondolewa kwa madai ya kuvamia eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Nyalandu, ambaye yuko ziarani mkoani Mbeya, jana alizungumza na wananchi na kuwahakikishia
Waziri Lazaro Nyarandu
kuwa Serikali haiwezi kuwaacha wakiangamia.
Akizungumza katika mkutano na  waandashi wa habari uliofanyika katika hotel ya Hill View jijini hapa alisema wananchi wanaoishi vijiji hivyo hawatahamishwa.

Alisema uamuzi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuitaka Serikali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo.
Alisema kwa muda mrefu mgogoro huo umekuwa ukitafutiwa ufumbuzi wa kudumu na umefika wakati ni lazima mambo yafikie mwisho ili wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo.

“Naomba niseme kuwa vijiji vinavyotakiwa kuhama vitaendelea kuwepo na ninaagiza kufanyika kwa ukaguzi wa mpaka katika GN 28 ili kuhakikisha haki inatendeka katika suala hili. Huu mgogoro ni lazima ufike mwisho na uamuzi huu una baraka zote za Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,” alisema Nyalandu.
 
Alisema maeneo yenye mgogoro mengi ndiyo kilimbilio na uchumi wa wananchi wa Mbarali kutokana na kuendesha shughuli za kilimo na makazi, hivyo Serikali haiwezi kuchukua uamuzi utakaokuwa na madhara kwa wananchi wake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo, alisema mgogoro huo umeleta mpasuko mkubwa na kusababisha wananchi kukosa imani na baadhi ya viongozi.
 
Naye, Mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi, alisema mgogoro huo umedumu kwa miaka mingi na ilikuwa ni lazima mwafaka ufikiwe ili kuleta amani na utulivu ulioanza kutoweka.





     Waziri Lazao Nyarandu akiongea na baadhi ya Waandishi wa Habari Hill view Hateli jijini Mbeya

0 comments:

Post a Comment