Maafisa wa kituo cha haki za binadamu(LHRC) watimuliwa na wakuu wa wilaya ya Rungwe na
Kyela baada ya kushindwa kujibu maswali yenye utata,hayo yamebainishwa na
ZAINABU MBUSSI mkuu wa wilaya ya Rungwe alipokua akiongea na mwandishi wa
habari hizi kujibu tuhuma zilizotolewa kwake kuwafukuza maafisa hao katika
wilaya yake.
![]() |
William Kahale |
“ niliwasimamisha kuendelea na zoezi la kuendesha mdahalo na
wananchi wa wilaya yangu kutokana na wao kushindwa kujibu baadhi ya maswali
yangu kitu ambacho kilinitia shaka juu ya elimu wanayotaka kuipeleka kwa Wananchi
wa Rungwe huenda haitakuwa sahihi.
![]() | ||
Mwassa Jingi |
Hali hiyo imejitokeza baada ya mmoja wa maafisa hao WILLIAM
KAHALE katika mkutano na waandishi wa habari mkoa wa Mbeya uliofanyika katika
ofisi za Mbeya Press Club zilizopo Soweto jijini hapa na kutoa shutuma kwa
wakuu wa wilaya hao kuzuia kufanya midaharo ya katiba pendekezwa katika wilaya
zao bila kupewa sababu za msingi.
“Nataka kuongea changamoto ambazo tumekutana nazo katika wilaya
mbili katika utoaji wa elimu ya katiba mpya kwa niaba ya Tume ya uchaguzi kwa
mujibu wa sheria kama tulivyopewa mamlaka kinyume na katiba ya jamhuri ya
Tanzania ibara ya 18 na 21 ibara ndogo ya pili kwa kua tumepewa huo uhuru, Sheria
ya kura ya maoni imeikaribisha Tume kutoa elimu ya uraia Tume imetupa majukumu
asasi za kiraia kutoa elimu kwa niaba yake,
wametuzia kwa makusudi na kuvunja sheria
ya uchaguzi” amesema KIHALEAwali Katika hali ya mchakato wa kuunda katiba mpya Sheria ya kura ya maoni imeipa mamlaka Tume ya uchaguzi kukaribisha Asasi za kiraia kutoa elimu ya uraia na kuziruhusu asasi za kiraia zaidi ya miatatu (300) kutoa elimu hiyo kikiwepo kituo cha sheria na haki za binadamu
Grace Mgonja Constitutional Trainer Sociologist (LHRC) akiongea na waandishi wa habari
Baadhi ya wananchi wa habari wakisikiliza kwa makini ndani ya mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment