Watu wenye ulemavu wa kusikia yaani Viziwi wameupongeza
uongozi wa Benki ya CRDB mkoa wa Mbeya kwa kuwapatia elimu ya ufunguaji na utunzaji wa pesa katika akaunti za Benki.
Shukrani hizo zimetolewa
na mwenyekiti wa Viziwi mkoan hapa TUSSA
MWALWEGA alipokua akiongea katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki
hiyo katika ukumbi wa Youth Center.
Tussa Mwalwega |
“Kumekuwepo na dhana potofu kwa jamii ya watanzania kwamba
sisi watu wanye ulemavu wa kusikia tupo tofauti na wengine na kwamba yapo mambo
ambayo haya tuhusu kitu ambacho si kweli sisi ni sawa na watu wengine na
tunastahili kuchukuliwa kama hao kwani ulemavu hatukupenda kuwanao i ila tunaushukuru
uongozi wa benki hii kwa namna ambavyo wamekubali na kuona umuhumu wa kutoa elimu hii kwetu” amesema Mwalwega.
Kwa upande wake STEPHAN MWAIPOPO ambaye alikuwa mkufunzi wa
semina hiyo amewataka walemavu hao kujitokeza kwa wingi katika kufungua akaunti
katika benki hiyo .
Mwaipopo amesema kuwa watawapunguzia gharama za kufungua kutoka elfu ishilini hadi elfu kumi tu, kwa kuw
a kunafaida nyingi ikiwepo utunzaji wa
pesa zao pamoja na mikopo midogo yenye riba nafuu itakayowawezesha kuendeleza biashara zao ndogondogo zitakazo wafanya wajikwamue
kiuchumi.
Naye meneja wa benki hiyo BENSON FRED amesema zoezi hilo
lilikua gumu kutokana kushindwa kuelewana kutokana na kutokua na uelewa wa lugha
ya alama ambayo wanatumia walemavu hao lakini kwa sasa wamepata mtu mwenye ujuzi wa
kutafsili lugha hiyo iameahidi kuendesha semina hiyo kwa wilaya zote za mkoa wa
Mbeya ili kuwahamsisha kufungua akaunti katika benki yeke.
Meneja wa Benki ya CRDG Benson Fred mwenye koti jeusi katika akiongea na watu wenye ulemavu wa kusikia VIZIWI kwa kutafsiliwa na mtaalamu wa Rugha ya alama FARAJA MBWILO katika semina hiyo
Mkufunzi wa Semina STEPHAN MWAIPOPO kutoka CRDB aliepo kushoto akifundishwa na kutafsiliwa na mkalimani Faraja MBWILO
Wanasemina kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mbeya wakiwa katika mafunzo
Lupi Mwaisaka Afisa Jinsia CHAVITA makao makuu akiongea jambo katika semina
Fadhili kwaleIsdory Mwashimaha
Tussa Mwalwega mwenyekiti wa CHAVITA Mkoa wa mbeya
Gwantwa Mugha
Severin Lwenagira
Tunganege Jackson
Washiliki wa semina wakiuliza maswali baada ya mafunzo
0 comments:
Post a Comment