Wananchi wametakiwa
kuwa na tabia ya kuweka mazingira yao katika hali ya usafi kwani ni swala muhimu katika maisha ya mwanandamu.
Wito huo umetolewana AYASY RAMADHAN operation
manager wa kampuni ya
ASAKYS INVESTMENT inayoshughurika na
usafi Mkoani Mbeya.
Ayasy Ramadhani Operation manager |
Amesema hayo
katika zoezi la uondoaji taka katika ghuba lililopo katika kata ya Sisimba
ambalo halijatolewa taka zaidi ya miezi sita na kusababisha usumbufu kwa wakazi
aeneo hilo kwa harufu mbaya na kutaka kuwahatalishia afya zao magonjwa ya milipuko.
“leo tupo
katika eneo hili la kata ya Sisima kwajili ya zoezi la kuweka mji wetu katika
hali ya usafi natoa wito kwa wakazi wa kata hii kutunza mazingira na kuyaweka
katika hali ya nzuri, kwani inawezekana kuishi bila uchafu tuige mikoa mingine wameweza kutunza mazingira yao”
amesema Ayasy
Ameongeza
kuwa swala hilo niendelevu kwa sasa wapo katika hatuo ya mwanzo katika
kuziondoa taka baada ya hapo wataweka vyombo maarumu vya kuhifadhia.
Aidha ametoa
angalizo kwa mtu yoyote atakae kutwa akitupa taka hovyo atakamatwa na kulipa
faini isiyopungua Tshs 50,000/=
Kwa upande
wake JOFREY KAJIGILI diwani wa kata ya hiyo amewataka wananchi wa kata yake
kutoa ushirikiano na kampuni ya ASAKYS INVESTMENT katika kufuata ratiba ya kuondoshwa taka
katika mitaa yao ili iwe rahisi kufanya kazi na kata yake iwe ya mfano wa
kuigwa na kata zingine, akitolea mfano mji wa moshi.
ASAKYS
INVESTMENT ni kampuni yenye makao yake mkuu jijini Mbeya inayo jishughulisha na
mambo ya usafi na kwa sasa imechukua tenda ya uondoswaji wa taka katika kata mbili ikiwepo ile ya forest.
Mwisho
Ayasi akiongea na waandishi wa habari
Jofrey kajigili diwani wa kata ya sisimba
Meneja na diwani wa kata ya sisimba wakionesha mfano katika kuwajibika kutekeleza swala la usafi
Gari la taka likipita katika kata ya Forest kukusanya taka
0 comments:
Post a Comment