Watanzania
wametakiwa kuipitia katiba pendekezwa kwa
makini kisha kuamua kuipigia kula ya
ndiyo au hapana.
Haya yamebainishwa na mwenyekiti wa jumuiya ya
wazazi chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Abdallah bulembo wakati akifungua shina la wazazi katika kata ya majengo jijini
Mbeya
Abdallah Bulembo |
Bulembo amesema
wananchi wasisikilize watu katika kutoa mawazo yao ya nini k katika ifanyike katiba
kwani kila mmoja anawajibu wakujua nini anapaswa kukifanya juu ya katiba
pendekezwa
Amesema
katiba inayopendekezwa ni kwa
mustakabali wa kizazi kijacho na
wanatakiwa kujua kuwa maamuzi yoyote mabaya yatakayo amuliwa ni mateso kwa
watoto wakizazi hicho.
“Ndugu zangu
ichukueni katiba pendekezwa isomeni vizuri na kuipigia kura ya ndiyo au hapana
hii ni kwa ajili ya watoto wenu nyie ya kwenu imeshapita miaka hamsini iliyopita
na miaka mingine ambayo sisi tutakua
tumekufa hivyo tusiamue kitu mabacho tutalaumiwa na vizazi vijavyo. Acheni
ushabiki katika kuamua kitu muhimu kama hiki” amesema Bulembo
Shina la wazazi lazinduliwa majengo |
Ameongeza kuwa
katiba hii ikipita itaanza kufanya kazi mwaka 2020 kwani kwa sasa bado katiba iliyopo itaendelea
kufanya kazi inaendelea kufanyiwa mchakato wa kuitengeneza, endapo itapigiwa
kura ya hapana itaendelea kutumika ile
ya zamani.
Pia
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura na uchaguzi wa viongozi unaotarajia kufanyika
mwaka huu .
Mwisho
Abdallah Bulembo akiwasili katika kata ya majengo na kusalimiana na viongozi wa kata hiyo
Katibu wa wilaya ya Mbeya mjini akiongea na wakazi wa kata ya majengo baada ya kuwasili katia soko la majengo.
Watoto hawakua nyuma
Bulembo awaongoza shangwe mamia ya wanachama wa (CCM) walojitokeza kumsikiliza katika soko la majengo kabla ya kuwahutubia
Viongozi mbalimbali walio ongozana na Bulembo wakiongozwa na mwenyekiti wa wazazi mkoa wa mbeya Fatuma Kassenga
Andrew Msaso mwenyekiti wa wazazi kata ya majengo akiongea kitu kwa mgeni rasmi
Islam Rajabu katibu wa wazazi mkoa wa mbeya akisoma risala mbele ya mgeni rasmi
Bulembo akihutubia wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa shina la wazazi katika kata ya majengo.
Bulembo akizindua shina la Regco
Bulembo akizindua kituo cha waendesha boadaboda wa majengo
Viongozi na wazee wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Bulembo akihutubia wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa shina la wazazi katika kata ya majengo.
Bulembo akizindua shina la Regco
Bulembo akizindua kituo cha waendesha boadaboda wa majengo
0 comments:
Post a Comment