Wakati harakati za
mashirika yasiyo ya Serikali yakiendelea kutoa elimu juu ya katiba pendekezwa
kablaya kupigiwa kura na kuwa katiba kamili, Mkurugenzi mtandaji wa Taasisi ya
mwalimu Nyerere JOSEPH BUTIKU amewataka wananchi kuipigia kura ya hapana katiba
pendekezwa.
Joseph Butiku |
Ameyasema hayo katika mdahalo uliofanyika katika ukumbi wa
chuo kikuu (TEKU) wakati wakitoa maoni
yaliyotolewa katika tume ya waryoba kwamba katiba hiyo haijazingatia kile
kilichomo katika rasmu hiyo.
elimu
ya uraia na kulinganisha
“Isomeni katiba vizuri na kuipigia kura ya hapana kwani
mkifanya hivyo italazimu kuipitia upya kutokana na kwamba katiba pendekezwa imeondolewa
maono yenu mengi ikiwepo mamlaka ya Raisi,
mbunge kuwajibishwa na wapiga kura wake, mawaziri wasitokane na wabunge nk”
wamefanya hivyo kutaka kutetea maslahi yao na kuwakandamiza wananchi” amesema
hayo Butiku
Na HANCE POLEPOLE amesema katiba ni mkataba kati ya wananchi
na viongozi wanao waongoza na hviyo wanatakiwa kuwa makini katika kutengeza
mkataba ili wasije laumiwa na vizazi
vijavyo kwa kushindwa kutengeneza katibayenye maslahi yao na
kuwafanya wengine watumwa katika nchi yao kwani kila mtu ana haki ya kufaidi kwa usawa.
Mwisho
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya mwalimu Nyerere akifungua madahalo katika ukumbi wa chuo kikuu (TEKU)
Hance polepole mmoja wa watoa mada akizungumzia kitu katika katiba pendekezwa
Ally Sarehe mmoja wa watoa mada
Pof: Mwesigwa Balegu mmoja wa watoa mada
Baadhi ya watu waliojitokeza kusikiliza mdahalo katika ukumbi wa chuo kikuu (TEKU)
Baadhi ya watu walipata fursa ya kuuliza maswali katika mdahalo huo
Kakulu mwandishi wa habari wa kituo cha Habari cha Azam Tv
0 comments:
Post a Comment