Wakosolewa kua wabinafsi wa kukumbatia kesi nyingi,
Wakili wa serikali mkuu Joseph Pande |
Katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria nchini,
mawakili wa kujitegemea wakosolewa wameonekana ndio chanzo cha kuchelewesha
mwenendo wa kesi mahakamani kwakua wamekua na ubinafsi na kulundikana na kesi
nyingi na hivyo kushindwa kumudu na kusababishe kesi kuchelewa kuisha kwa
wakati.
Hayo yamebainishwa na wakili wa serikali mkuu mfawidhi wa
ofisi ya mwana sheria mkuu JOSEPH PANDE alipokua akitoa taarifa ya mwenendo wa
kesi kwa mwaka ulio pita 2015 katika kilele cha sherehe za wiki ya sheria
zilizo fanyika katika ukumbi wa mkapa jijini Mbeya
PANDE amesema kumekuwepo na sababu nyingi zinazo sababisha
kesi kuchelewa kuisha kwa wakati katika mahakama zetu ikiwa ni pamoja na
mawakili hao kukumbatia kesi nyingi kwa wakati mmoja na kusababisha hakimu
kuahilisha kila wakati kusikiliza kesi kutokana na mawakili wa kujitegemea
kushindwa kumudu muda kwa sababu ya mlundikano wa kesi zao.
“Mahakama imejitahidi kumaliza kesi zote zilizo fika
mahakamani hapo kusikilizwa, Kesi zilizo baki ni zile zinazo endeshwa na mawakili wa kujitegemea wamekua wabinafsi
sana katika kazi zao hawataki kugawana ili waweze kumudu na kuzimaliza kwa muda
muafaka, Ninawashauri waanzishe makampuni ambayo yatakua na mawakili wengi
hivyo kumudu kesi zote kwa muda muafaka” amesema PANDE
Ameongeza kua sababu zingine zinazo sababisha ucheleweshwaji
wa kesi mahakamani ni pamoja na vyombo vya upelelezi kushindwa kuharakisha
upelelezi kwa wakati, mambo mengine ni
pamoja na waendesha mashitaka kutojipanga kuleta mashahidi mahakamani kwa muda muafaka na mambo mengine
mengi.
Nae Jaji mfawidhi kanda ya Mbeya NOELI CHOCHA amempongeza
raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya tano JOHN POMBE MAGUFURI
kwa juhudi zake za wazi kwa huduma za serikali yake zenye kusudi la kumlenga
mwananchi moja kwa moja katika kuletea maendeleo sana wale wa kipato cha chini.
“Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza raisi kwa juhudi
zake za wazi kwa huduma za serikali yake kumlenga mwananchi moja kwa moja
kwakua serikali bila mwananchi ni uhaini na udikteta hivyo huduma za serikali
kumlenga mwananchi ni haki kwakua ndiyo waliyo iweka madarakani” amesema
CHOCHA.
Kwa upoande wake mgeni wa heshima wa sherehe hizo mkuu wa
mkoa wa Mbeya ABBAS KANDORO amewapongeza
watumishi wa mahakama kwa jinsi walivyo anziaha mahakama ktika mji wa chapwa
wilayani momba na amewataka waanzishe mahakama nyingine mkwajuni wiy a ya
chunya mkoani mbeya.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas kandoro akiongea na wadau wa sheria
Jaji mfawidhi kanda ya Mbeya akikagua gwalide kabla ya kuelekea katika ukumbi wa mkapa kwa ajili ya sherehe.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliepo katikati ya majaji akiongoza maandamano kuelekea ukumbi wa mkapa.
Baadhi ya mahakimu na mawakili wa serikali na wa kujitegemea walio shiriki maadhimisho ya sherehehe
Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama
Viongozi wa dini
Watumishi wa mahakama na polisi
Kwaya ya mahakama ikitumbuiza katika sherehe za siku ya sheria nchini
0 comments:
Post a Comment