
MJASILIA MALI JOTHAM MWANDIBWA AKIZUNGUSHA MASHINE YAKE KUKAMUA MIWESE
Katika hali ya kukabilia na naisha kijana aliejulikana kwa
jina la Jotham Mwandibwa ameziomba asasi na mashirika mbalimbali yenye uwezo wa
kumkopesha mashine ya kukamua mafuta ya mawese ya kisasa, ili kuboresha
biashara yake hiyo ili aweze kumudu kutunza famila yake.
Mwandibwa ameyasema hayo alipotembelewa na mwandishi wa Blog
hii kiwandani kwake ambako anendesha shughuli za ukamuaji wa mafuta hayo kwa mashine ya kienyeji, iliyo jengwa kwa
pipa la bati ndani yake kukiwa na vipande vya nondo vinavyowezesha kusaga na
kubangua mbegu za muwese na kupatikana kwa mafuta ya kupikia na sabuni za
kufulia .
“Ninaomba Tasisi au shirika lolote linaloweza kuniwezesha
kupata mashine ya kisasa itakayoweza nisaidia kuboresha mradi wangu huu wa
kukamua mafuta ya mawese ili niweze kumudu kupambana na maisha kwani biashara
yangu inawateja wengi lakini mashine hii duni nashindwa kumudu soko, nikipata
mtu wa kunikopesha mashine ya kisasa itaniwezesha kufanya kazi hii kwa ufanisi
zaidi” amesema mwandibwa.
Mwandibwa mwenye familia ya mke na watoto sita ambao ni
mapacha matatu anae ishi kijiji cha Lwifwa kata ya kisiba wilaya ya Rungwe
Mkoani mbeya amekua akitegemea biashara yake hiyo kuendesha na kutunza familia yake.
HATUA YA KWANZA NI KUCHEMSHA KABLA YA KUKAMUA MAFUTA
ROBERT SOKAPO AKIMSAIDI BABA YAKE KUFANYA USAFI ENEO LA KUKAMULIA MAFUTA
SHUGHURI YA UKAMUAJI INAENDELEA
BAADA YA KUKAMULIWA MAFUTA HAYO HUJAZWA KATIKA PIPA NA KISHA KUENGU YALIYOIBUKA JUU KAMA UNAVYO MUONA MAJASILA MALI HUYU
BAADA YA KUENGULIWA HURUDISHWA TENA KATIKA MOTO ILI KUPATA MAFUTA HALISI
BAADA YA MUDA HUIPULUWA NA TAYALI MAFUTA YA MAWESE YAMEPATIKANA
BAADA YA KUPOA MAFUTA HUCHUJWA
MAWESE YAMEKAMULIWA NA KUCHUJWA VIZURI YAPO TAYALI KWA MATUMIZI YA KUPIKIA

MABAKI YA MAPEKE YA MAWESE HUBANGULIWA NA HUKAMULIWA MAFUTA TENA AMBAYO HUTUMIKA KUTENGENEZA SABUNI.
KAZI YA KUKAMUA MAFUTA IMEKAMILIKA NASASA TAYALI KWENDA SOKONI
0 comments:
Post a Comment