DIWANI WA KATA YA MAENDELEO KUPITIZ CCM PANTALEO SHIO AKIONGEA NA WAFANYA BIASHARA WA SOKOMATOLA
MFANYA BIASHARA AUSONY MTOKOMA AKIONGEA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
JOHN CHUNGWA AKITOA KERO YAKE KATIKA MKUTANO
MFANYA BIASHARA BEN JOSHUA MUHANGA WA KUWEKEWA SUPER GLUE KATIKA KUFULI LA MLANGO WAKE AKITOA SHUTUMA KWA MWENYEKITI WA SOKO HILO KUA NDIYE MHUSIKA MKUU WA JAMBO HILO
MKUU WA SOKO OLIVA AMBELE AKIFAFANUA JAMBO
![]() |
| MFANYA BIASHARA JOYCE MWAKASOLE AKITOA KERO YAKE |
MWNYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA SOKOMATOLA AKIONGEA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
BAADHA YA WAFANYA BIASHARA WALIHUDHULIA MKUTANO HUO
HABARI
PANTALEO SHIO DIWANI WA KATA YA MAENDELEO KUMALIZA
MGOGOLO SOKOMATOLA
Akiongea katika na wafanya biashara wa soko hilo kwenye
mkutano wa pamoja wenye lengo la kutaka
kujua changamoto zinazo wakabiri wafanya biashara hao Shio amewataka watoa kero
zilizopo katika soko hilo ili kuzidafutia ufumbuzi na kuleta amani na utulivu
katika soko.
“Mimi kama diwani wenu nimeitisha kutano huu ili kuchukua changamoto
na kero zenu ambazo zinawakabiri katika soko hili nimesikia mambo mengi sasa basi
kupitia mkutano huu nawataka kila mmoja wenu kusema kila kilichopo katika moyo
wake ili tuweze kulitatua na kulimaliza kabisa tatizo lililopo hapa kusudi
tufanye biashara kwa amani upendo na utulivu kwakua sisi wote hapa ni ndugu”
amesema Shio
Akiongea mmoja wa wafanya biashara hao Ben Joshua amesema
katika soko hilo kumekuwepo na mgogoro mkubwa kati yabaadhi ya wafanya biashara hao na mwenyekiti wa soko
hilo Abdallah Shaibu kutokana na itikadi ya vyama jambo ambalo limeleta uhasama
mkubwa kati yao na kuligawa pande mbili soko hilo.
Ameongeza kua uhasama huo ambao uliitwa kwa majina tofauti
wengine wakisema waunguja na wapemba na wangine wakisema maalshababi umefikia
pabaya kufikia kumshutumu kiongozi huyo kutia Super glue katika makufuri ili
kushindwa kuyafungua.
Nae John chungwa amesema chanzo cha mgogoro huo ni siku
iliyo fanyika usafi kitaifa kwa amri ya Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John pombe magufuri
kuamuru Tarehe 09dec 2015 kwamba badara kuadhimisha sikuku ya uhuru basi siku
hiyo itumike kufanya usafi katika maeneo yetu.
Ndipo wafanya biashara wa soko hilo walijiwekea sheria ndogo
ya kwamba endapo mtu hata fika ama kuchelewa kufika kufanya usafi basi kutakua
na adhabu ya kulipa pesa kiasi cha shilingi elfu mbili kitu ambacha baadhi yao
hawakutekeleza sheria hiyo.
Kwa upande wa Mwenyekiti Abdallah Shaibu ambae ndiye
aliyetuhumiwa kuanziaha mgogolo huo amekili kuwepo kwa tofauti hizo kati yake
na kundi hilo aliloliita alshababi kwamba imetoka na wafanya biashara hao kuto
kubaliana na uongozi wake hivyo wamekua wakifanya visa mbalimbali ili kuungusha
utawala wake
“Ni kweli mgogoro huo upo ambao umesababisha na kundi la
alshababi kutokubaliana na uongozi wangu, Ninao ushahidi wa barua iliyo andikwa
na kikundi hiki kwamba hautakuakua tayali kushirikiana na uongozi huu kwa hiyo
sioni ajabu kwa tuhuma hizi zi naziendelea zina lengo la kunichafua” amesema
Shaibu
Kuhusu tuhuma za yeye kuhusika na utiaji Super glue katika
makufuli ya wa baadhi ya maduka ya wafanya biashara hao Shaibu amekanushakua
hakuhusika na kuwataka wanao mtuhumu
kuleta ushahidi na kama itadhibitika kua kahusika basi yeye yupo tayali
kujiudhuru nafasi hiyo.
MWISHO

















0 comments:
Post a Comment