Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amezindua warsha ya siku moja ya uraghabishi na
uhamasishaji juu ya magojwa yaliyokua hayapewi kipaumbele iliyofanyika katika
ukumbi wa mkapa jijini hapa
Warsha hiyo iliyo andaliwa na wizara ya afya na maendeleo ya
jamii, jinsia, wazee na watoto kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa
yaliyokua hayapewi kipau mbele ime jumuisha wadau kama wakuu wa wilaya,
Wakurugenzi wa Halmashauri, maafisa elimu na madaktali.
Akiongea katika warsha hiyo Kandoro ame wataka viongozi hao
kusimamia kwa ukamilifu zoezi la umezeshaji dawa kwa kinga tiba ya magojwa haya
ili mkoa wa Mbeya kwa mwaka huu na miaka ijayo iondokane na magonjwa yasiyo
pewa kipaumbele.
“Rai yangu kwa Wakuu wa wilaya Wakurugenzi wa Halmashauri na
viongozi wa ngazi zote kusimamia kikamilifu zoezi la umezeshaji dawa kinga tiba
ya magonjwa haya ili mkoa wetu mwaka huu na miaka ijayo uweze kupata “Coverage”
ya umezaji dawa” amesema Kandoro
Ameongeza kua Wakurugenzi wa Halmashauri mpango huu waingize
katika mipango yao na kutenga pesa za kutosha za kupambana na magonjwa haya
badala ya kutegemea pesa za wahisani tu.
Lakini pia amewaasa Wakurugenzi na maafisa wote wanao husika
na mchakato wa kutoa pesa hizi za mradi waache ukilitimba ili pesa hizo zitoke
kwa wakati na kuwezesha shughuri hii kufanyika kwa wakati ulio pangwa.
Kwa upande wa wananchi Kandoro amewataka kujitokeza kwa
wingi ili kumeza dawa hizo za Kinga tiba kama watakavyo elekezwa na wataalamu
wakati wa kampeni husika. Amesema dawa hizi zimethibitishwa na Shirika la Afya
nchini kua ni salama na hazina madhara yoyote.
Mkoa wa Mbeya umezeshaji wa dawa hizi za Mectizan na
Albendazole kwa kinga tiba ya magojwa ya Matendena mabusha utafanyika tarehe 20
mwezi huu wa Februari na pia utafanyika umezeshaji wa dawa ya Praziquatel na
Albendazole kwa ajilia ya kinga tiba ya minyoo pamoja na kichocho kwa watoto walio na umri wa kwenda shule ugawaji
huu utafanyika mashuleni mwezi wa agosti
kwa mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akifugua warsha
Muwezashaji wa warsha Edward Kirumbi Program officar NTD Program wizara ya Afya akileza jambo kuhusiana na matumizi ya dawa.
Muwezeshaji wa warsha Dr Boniphace Idindili Envision Program manager akisema neno katika semina hiyo
Baadhi ya washiriki waliopata nafasi ya kujitmbulisha
Edward Kirumbi muwezesha wa warsha
Afisa Elimu mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila akichangia mada katika warsha
Mganga mkuu mbarali Dr Boniface Kasululu akichangia mada
0 comments:
Post a Comment