Wananchi na
Wakazi wa Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, mapema leo
wamefunga barabara ya Mwanza-Musoma katika eneo la Kisesa na hivyo
kusababisha abiria wanaoingia Jijini Mwanza kutoka Mikoani kukwama
barabarani kwa zaidi ya masaa manne.
Wamechukua maamuzi hayo baada ya dereva
wa daladala moja kuwagonga wanafunzi wawili wa shule ya msingi Isangijo
na kusababisha mmoja kufariki dunia papo hapo.
Baada ya hatua hiyo, jeshi la polisi,
kikosi cha kuzuia ghasia limefika eneo la tukio na kuwasihi wananchi
kufungua barabara hiyo ili kutowakwamisha abiria kuendelea na safari
zao.
Picha na Mdau @BMG
Wananchi wakiwa
wamefunga barabara ya Musoma-Mwanza, katika eneo la Kisesa baada ya
daladala kuwagonga wanafunzi wa shule ya msingi Isangijo katika eneo
hilo.
Askari wa kutuliza ghasia wakia eneo la tukio
Askari wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio wakijaribu kuondoa mawe barabarani.
0 comments:
Post a Comment