Mkurugenzi
wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kulia), kwa
niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, akimkabidhi kiongozi wa
wagonjwa wa ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Francis Yango
(kushoto), dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.milioni 5
vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Dar es
Salaam leo asubuhi. Wapili kulia ni Muuguzi wa zamu,Getrude Massawe na
Antusa Lasway.
Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa mbele ya vifaa na dawa walivyotoa msaada kwa Hospitali hiyo.
Hapa ni furaha tupu kabla ya kukabidhi msaada huo.
Makabidhiano zaidi ya msaada huo ukitolewa..
mwonekano wa maboksi yenye msaada huo baada ya kupokelewa.
Vifaa hivyo vikipelekwa kwa walengwa.
Mkurugenzi
wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kushoto),
akimkabidhi dawa za meno na sabuni, Judith Kimei katika wodi ya wazazi.
Kulia ni Muuguzi wa zamu Antusa Lasway.
Ofisa wa benki hiyo, Neema Tumsifu akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Ofisa wa benki hiyo, Valentina Chesama akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiyo.
Wafanyakazi hao wa Bebki ya Azania wakiondoka Hospitalini hapo baada ya kukabidhi msaada huo.
Na Dotto Mwaibale
BENKI
ya Azania imetoa msaada wa dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya
sh. milioni 5 wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala
jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo wakati wa kukabidhi
msaada huo Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa Mikakati na
Biashara, Mwanahiba Mzee alisema kila mara benki hiyo imejiwekea
utaratibu wa kusaidia jamii kulingana na ratiba yao ambapo mwaka huu
waliona ni vema msaada huo waupeleke Hospitali hiyo.
Alisema
mwaka katika kusherehekea sikukuu ya wanawake waliona ni vema kutoa
msaada hasa katika wodi ya wajawazito ukizingia kuwa sikukuu hiyo
inawahusu.
"Tumetoa
msaada wa dawa mbalimbali kama dettol, spiritis, mabomba ya sindano,
micoprostol, vitamini k na nyingine nyingi pamoja na vifaa vya usafi
kama vile mifagio, sabuni na dawa za mswaki" alisema Mzee.
Kiongozi
wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali hiyo, Francis Yango akizungumza
wakati wa kupokea msaada huo kwa niaba ya Mganga Mkuu, Shadrack Shimwela
aliishukuru benki hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia.
"Tunawashukuru
sana Azania Bank Ltd kwa msaada wenu lakini tunawaomba muende mbele
zaidi kama mtaweza mtujengee walau wodi ambayo itaingiza walau vitanda
30 na wodi hiyo muandike jina la benki yenu kwani changamoto kubwa
tulionayo kwa sasa licha ya kuwa na vitanda vya kutosha tuna uhaba wa
wodi" alisema Yango.
The Perfect Casino: Top Offers & Bonuses at
ReplyDeleteThe Best Casino Offers. septcasino Casino Bonuses & Promotions. With an gri-go.com emphasis on febcasino casino games, https://vannienailor4166blog.blogspot.com/ the gambling https://septcasino.com/review/merit-casino/ industry is expected to explode