Na Mwandishi wetu
Chama
cha Wakunga Tanzania (Tanzania Midwives Association-TAMA) imefanya
mkutano maalum wa kuhamasisha waandishi wa Habari kuhusu kazi za wakunga
katika kuelekea siku ya Wakunga Dunia ifikapo hapo Mei 5 mwaka huu.
Katika
mkutano huo uliofanyika jana Aprili 28, TAMA ilibainisha kuwa,
wanahabari wengi wamekuwa wakichanganya habari za wakunga wataalam
ambao wapo chini ya Chama hicho na wale wakunga wa jadi ambao hawana
taalum pamoja na kiapo cha kufanya kazi hiyo kitu ambacho kinaleta
usumbufu mkubwa kwa jamii.
Mratibu
wa TAMA, Bi. Martha Rimoy katika mkutano huo, ameeleza kuwa, shughuli
za Wakunga wataalam ni wale tu ambao wamesomea taaluma hiyo pamoja na
kula kiapo katika kumsaidia Mama na Mtoto na na huyo ndiyo anaitwa
Mkunga na si wale ambao hawajapata mafunzo wala kula kiapo.
Katibu
Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari (kushoto) akieleza jambo kwa
wanahabari na watu mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo kwa
waandishi wa habari juu ya kufahamishwa shughuli za Wakunga. Kulia ni
Bi. Felister Bwana kutoka UNPFA, Nchini Tanzania.
Mkutano huo ukiendelea...
Baadhi ya maafisa kutoka taasisi za Wakunga na mambo ya Afya wakifuatilia mkutano huo.
..................
Aidha,
aliomba wanahabari na vyombo vya habari kuzipatia nafasi/Kipaumbele
habari za Wakunga kwani zitaondoa woga kwa jamii iliyojenga Imani potofu
kwa wakunga.
“Jamii imekuwa ikijenga Imani potofu namna ya Wakunga buka kujua mkunga huyo ni yupi.
Tunaomba
ifahamike Mkunga ni yule aliyepata mafunzo yake kitaalam na pia kula
kiapo pamoja na kusajiliwa na taasisi husika kama ilivyo taratibu za
Nchi.
Tuondoe
Imani zingine kwa Wakunga pia tunawaomba wanahabari kuweza kutoa elumu
ya kutosha kuhusiana na mambo ya Wakunga hasa wakunga wataalam ambao
wamepatiwa mafunzo yote ya kuhakikisha wanamuokoa Mama na mtoto wakati
wa uzazi” alieleza Bi. Martha Rimoy.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika mkutano huo, ameeleza kuwa, Wakunga wataalam wanao
wajibu
wa
kumsaidia Mwanamke na mtoto katika kukabiliana na vifo vitokanavyo na
Masuala ya Uzazi vinavyozidi kuwatesa akina mama wengi, hasa inapokuja
wakati wa tendo la kujifungua.
Aidha,
Dkt. Sebalda amebainisha kuwa, pamoja na Changamoto mbalimbali, vifo
vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5, imepungua kwa asilimia 81,
huku akitaka muendelezo wa elimu utolewe kwa Jamii.
Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akito mada katika mkutano huo..
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akitoa mada katika mkutano huo kwa wanahabari..
..............
Kwa
upande wake, Afisa Mipango wa Afya ya Mama na Uzazi wa Shirika la Idadi
ya Watu Duniani (UNFPA)nchini, Bi. Felista Bwana ameelezea kuwa, upo
umuhimu wa Mkunga mtalaam katika kuokoa Uhai wa Mama na mtoto kwani bila
wao Dunia ingekuwa kwenye matatizo makubwa.
Siku
ya Ukunga Duniani Inatarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi
mmoja Jijini Dar es Salaam, Mei 5 mwaka huu huku ikibeba ujumbe wa kauli
mbinu ya “Wanawake na Watoto wachanga ni muhimili wa Ukunga”.
Aidha,
mkutano huo ulieza changamoto wanazokabiliana nazo wakunga ni nyingi
hivyo wameimba Serikali kuangalia namna ya kukabiliana nayo ili kila
Mkunga kufanya kazi yake kwa uhuru na haki kwa dhama za sasa huku
wakiomba jamii kuondoa dhana potofu dhidi yao pindi wawaonapo katika
vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali zote.
Mkutano
huo maalum wa TAMA, ulihusisha wanahabari mbalimbali kutoka katika
vyombo vya Habari nchini ikiemo, Magazeti, Radio, Televisheni na
magazeti ya mtandaoni.
Mratibu
wa TAMA, Bi. Martha Rimoy akitoa mada maalum kwa waandishi wa habari
namna kazi na shughuli za Wakunga wanazofanya hapa nchini.
Afisa Mipango wa UNFPA, hapa nchini, Bi.Felista Bwana akitoa maelezo mafupi juu ya wakunga hapa nchini.
Mratibu wa TAMA, Bi. Martha Rimoy akitoa mafunzo hayo katika mkutano huo kwa wanahabari.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Bi. Felista Bwana akitoa mada katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akifafanua maswali kwa wanahabari wakati mkutano huo..
Picha
ya pamoja baadhi ya wanahabari na wandaaji wa mkutano huo maaalum kwa
wanahabari kuelekea siku ya Wakunga Duniani ambayo kilele chake ni hapo
Mei 5 mwaka huu huku kwa Tanzania ikitarajiwa kufanyika kwenye viwanja
vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment