Pages

Ads 468x60px

Sunday, May 1, 2016

Mkutano wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika Wafanyika Jijini DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo umeandaliwa na Jopo la Ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alilolituewa Mwanzoni mwa huu, kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Jopo la ngazi ya Juu la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kuwezesha wanawake kiuchumi Baada ya kufungua mkutano kuhusu kuwezesha wanawake kiuchumi katika nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika. Mkutano huo unazungumzia kuhusu kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekezo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ifikapo 2030. 
(Picha na OMR)

0 comments:

Post a Comment