![]() |
Haji
Kihwele kutoka shirika la Oxfam akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi hati za hakimiliki za kimila zilizofanyika katika kijiji cha
Nyida.
|
![]() |
Mkurugenzi
wa SHIDEPHA+ Venance Muzuka akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi
hati za hakimiliki za kimila zilizofanyika katika kijiji cha Nyida.
|
![]() |
Wakazi wa kijiji cha Nyida wakihudhuria hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila.
|
![]() |
Wakazi wa kijiji cha Nyida wakiangalia hati zao walizopokea.
|
![]() |
Wakazi wa kijiji cha Nyida wakihudhuria hafla ya kukabidhi hati za hakimiliki za kimila. .............. |
MKUU
wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amekabidhi jumla ya hati za
hakimiliki za kimila 92 kwa wakazi wa kijiji cha Nyida mkoani Shinyanga.
Hatua
hiyo ya ugawaji wa hati ilifanyika hivi karibuni katika Wilaya hiyo,
baada ya viwanja vya wakazi hao kupimwa na kupatiwa mafunzo ya matumizi
bora ya ardhi.
Alisema
Hati hizo zitawasaidia wananchi kupunguza au kuondoa kabisa migogoro ya
ardhi katika wilaya hiyo kwa sababu watakuwa wanamiliki maeneo yao
kisheria.
Matiro
alisema migogoro mingi ya ardhi inatokea kutokana na watu kutokuwa na
hati zinazoonyesha ukubwa wa maeneo yao na kusababisha mgogoro baina ya
mtu na mtu.
Matiro
aliwapongeza maafisa ardhi kwa kuweza kufanya kazi hiyo kwa kutumia
shilingi milioni tatu kwa kila kijiji tofauti na milioni tisa
iliyoelekezwa na serikali.
“Natoa
shukrani zangu za dhati kwa ushirikiano mkubwa na ufadhili kutoka kwa
wadau wa maendeleo ikiwemo Shirika la Oxfam na SHIDEPHA+ kwa kusaidia
kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi ili wananchi wa wilaya yangu
kufahamu umuhimu wa hati hizo,” alisema.
Kwa
Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,
Kiomoni Kibamba alisema kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Oxfam na
SHIDEPHA+ wamefanikiwa kutekeleza mradi wa kuandaa mpango wa matumizi
bora ya ardhi ndani ya vijiji vinne ambavyo ni Shabuluba, Nyida, Mwenge
na Puni.
Alisema mradi huo ulianza mwezi wa Februari 2016 na sasa upo katika hatua za mwisho za utekelezaji katika vijiji hivyo.
Alitaja
changamoto mbalimbali za kupata haki miliki za kimila kuwa ni pamoja
na ukosefu wa rasilimali fedha ndani ya jamii, baadhi ya wananchi
kugubikwa na umaskini na kukosa fedha kwa ajili ya kuchangia gharama za
upimaji.
Kibamba
alisema changamoto nyingine ni pamoja na kukosekana kwa vigezo elekezi
vya Wizara na kanuni ya sheria ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 kuhusu
kupatiwa hati miliki ndani ya serikali za vijiji ambavyo ni pamoja na
kukosa ofisi zenye hadhi za Halmashari za vijiji pamoja na ukosefu wa
masijala za ardhi na daftari za ardhi za vijiji kwa ajili ya usajili wa
Hakimiliki za kimila.
“Faida
zilizotokana na mradi wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika
halmashauri ni pamoja na uhamasishaji na utoaji wa elimu juu ya hati za
haki miliki za kimila uliotolewa kwa vijiji vinne pamoja na kupunguza
na kutokomeza kabisa migogoro ya ardhi ndani ya jamii katika vijiji
husika,” alisema Kibamba.
Alitaja faida
nyingine kuwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira kwa kupanga matumizi
sahihi ya ardhi ndani ya mipaka ya kijiji, umiliki wa ardhi kisheria
ndani ya jamii kwa wananchi kupatiwa hati za hakimiliki za kimila pamoja
na jamii kupata uwezesho wa kifedha kutoka taasisi za kifedha baada ya
kupatiwa hati miliki.
Nae miongoni
mwa wakazi waliopokea hati hizo ambae ni Mkazi wa Kijiji cha Nyida,
Flora Nkingwa alishukuru kukabidhiwa hati hizo kwani sasa anamiliki eneo
lake kisheria.
Nkingwa alisema eneo alilopatiwa hati lina ukubwa wa nusu ekari ambalo analitumia kwa kilimo cha Mahindi na Karanga.
Hati hizo za
bila kikomo zilitolewa kwa mchanganuo wa hati 75 za familia, hati 7 za
wanawake, hati 5 za wanaume, hati 2 za Taasisi na hati 3 za ukoo.
0 comments:
Post a Comment