Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
29/07/2016
Dar es salaam
Watumishi
 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
wamechangia kiasi cha Tsh. Milioni 100 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha 
umma kuhusu zoezi la upatikanaji wa madawati katika shule za msingi na 
Sekondari nchini.
Akikabidhi
 mchango huo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa niaba ya watumishi
 wa wizara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika 
Mashariki Balozi  Augustine
 Mahiga amesema kuwa watumishi hao wametoa fedha hizo kwa shule ya 
msingi Chamazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la upatikanaji wa 
madawati katika shule za msingi na sekondari nchini. 
Balozi
 Mahiga amesema Wizara yake iliwahamasisha watumishi wake walio makao 
makuu na wale walio kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi kuchangia zoezi
 hilo la upatikanaji wa madawati.
“Ili
 kufanisha upatikanaji wa fedha hizi Wizara yangu iliwahamasisha 
watumishi wake wote walio Makao makuu na wale walio katika balozi zetu 
duniani kote,  wito
 huu uliitikiwa kwa ari na hamasa kubwa na kufanikisha kukusanya kiasi 
cha Shilingi 100,176,825.52 za kitanzania”alisisitiza Balozi Mahiga 
Waziri
 Mahiga aliongeza kuwa mara baada ya kukusanya fedha hizo watumishi wa 
Wizara hiyo waliamua kumpatia aliyekuwa Mtumishi wa Wizara ambaye sasa 
ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni kiasi cha shilingi Milioni 15 
kwa ajili ya ununuzi wa madawati katika Wilaya yake.
Aidha, amesema kiasi fedha zilizobaki zaidi ya shilingi milioni 85 zilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa  kwa ajili ya mchango wa utengenezaji wa madawati ya shule ya Msingi Chamazi iliyoko Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
Waziri
 Mahiga aliongeza kuwa mbali na wizara yake kuwa na majukumu mbalimbali 
bado inalo jukumu la kuhakikisha inaitangaza Tanzania ili kuvutia 
wawekezaji na kukuza uchumi wa nchi, na kuongeza kuwa elimu bora ni 
msingi imara katika kufanikisha hilo.

0 comments:
Post a Comment