Mkazi
wa Kijiji cha Ndubi kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Julius
Mwambola (kulia), akionyesha migomba iliyoangushwa kutokana na mvua
iliyonyesha wilayani humo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni mke wake
Nabwike Swebe.
.............................
.............................
Dotto Mwaibale, Mbeya
Wakazi
wa Vijiji vya Ndubi, Mpuguso Kata ya Kisondela Tarafa ya Pakati
wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na
upepo ambayo imeezua baadhi ya mapaa ya nyumba na kuangusha migomba.
Akizungumza
kuhusu tukio hilo mkazi wa Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi alisema
wamepata pigo kubwa kutokana na mvua hiyo iliyonyesha mwishoni mwa wiki
kutokana na migomba mingi kuanguka hivyo kutishia tishio la njaa.
"Siwezi
kuelezea kwa undani tathmini ya athari ya mvua hii lakini tumepata pigo
kwani kaya nyingi migomba imeangushwa na mvua hiyo" alisema Mwangosi.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho Julius Mwambola alisema mvua hiyo imeangusha migomba yake 100 yenye thamani ya sh.250,000.
"Tumeathiriwa
kwa kiasi kikubwa na mvua hii kwani mimi binafsi migomba iliyoangushwa
na upepo wa mvua hiyo ni zaidi ya 100" alisema Mwambola.
Mkazi
mwingine wa Kijiji cha Mpuguso kitongoji cha Nkuju, Tulinagwe Naswila
alisema mvua hiyo imeangusha migomba yake 40 yenye thamani ya
sh.200,000.
Alisema
mvua hiyo ilianza kunyesha saa saba mchana na ilidumu kwa muda wa saa
moja na kuleta athari kubwa ya kubomoa baadhi ya nyumba na kuharibu
migomba.
"Mvua
ilikuwa kubwa ambayoiliharibu migomba na kuezua paa za nyumba kadhaa na
kubomoa nyumba ya mjane mmoja aliyemtaja kwa jina la Gwanaloli Ndapapa
(85).
Jitihada
za kumpata Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Chalya ili kuzungumzia
suala hilo zilishindikana baada ya kupigiwa simu mara kadhaa bila ya
kupokelewa.
Migomba ikiwa imeanguka kutokana na mvua hizo.
Mwanahabari Dotto Mwaibale, akichukua taarifa ya athari ya mvua hiyo kutoka kwa mkazi wa Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi.
Nyumba ya Kikongwe, Gwanaloli Ndapapa ikiwa imeezuliwa paa na mvua hiyo ya upepo.
Kikongwe
Maria Kamendu (85), akiwa ameshika paa la nyumba ya jirani yake
Gwanaloli Ndapapa iliyobomolewa na mvua iliyonyesha mwishoni mwa wiki
katika Kijiji cha Ndubi wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kuharibu migomba
na baadhi ya nyumba.
0 comments:
Post a Comment