Australia imesema itaongeza hadi watu 20,000
kila mwaka idadi ya wakimbizi itakayowapokea nchini humo, ikiwa ni nyongeza ya
asilimia 40, na nyongeza kubwa kabisa tangu kupita miaka 30.
Hatua
hiyo ni mpango wa kuzuia watu kuingia nchini humo kwa magendo. Waziri Mkuu wa
Australia, Julia Gillard, amesema mpango huo pia utawapa hifadhi wakimbizi
400 kutokea Indonesia, kama ishara ya nia njema. Awali Australia ilikuwa
inachukua wakimbizi 13,750 kwa mwaka. Australia sasa imesema itashauriana
na shirika linalowashughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa na washirika wake
wengine, huku waziri wa uhamiaji, Chris Bowen, akisema wakimbizi wengine
watakaohifadhiwa ni wa kutoka Mashariki ya kati, Kusini Mashariki mwa Asia na
Afrika. Hatua hii itaifanya Australia kuwa taifa la pili duniani kuwapatia
makazi idadi kubwa ya wakimbizi baada ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment