Pages

Ads 468x60px

Sunday, December 1, 2013

Elizabeth Mwakijambile, mshiriki anayeshangaza


 

  002-2 

 SONY DSCEBSS :Elizabeth Mwakijambile, mshiriki anayeshangaza kwa uwezo wa ziada wa kuimba sauti ya kiume, msikilize hapa


Kipaji, uwezo na bidii katika biashara ya muziki ni vitu ambavyo vikiunganishwa vinaleta kitu kikubwa, lakini pia kuna vitu vya ziada ambavyo msanii anakua navyo kutokana na kubarikiwa tu na Mungu sio kwa juhudi zake za kukitafuta.

Elizabeth Mwakijambile, mshiriki wa shindano la kuimba la Epique Bongo Star Search 2013 ana kitu cha ziada ambacho amebarikiwa ambapo msanii huyu ana uwezo mkubwa wa ku-switch sauti na kuimba vizuri sauti ya kiume kiasi kwamba kama mtu hamuoni na hamfahamu anaweza kuamini kabisa kuwa anaeimba sio tu ni mwanaume bali ni msanii mzuri wa kiume.

Elizabeth amekutana na kinasa sauti cha tovuti na Times fm, na kuonesha uwezo huo aliojaliwa na mwenyezi Mungu.

“Mimi ndiye mshiriki pekee wa EBSS 2013 ninaeweza kuimba kwa sauti ya kiume na ya kike, nimebarikiwa tu.” Alijigamba Elizabeth wakati anaongea na tovuti ya Times fm.

Mshiriki huyu namba 08 wa shindano hilo, ni kati ya washiriki watano walioingia fainali zitakazofanyika November 30 mwaka huu, katika ukumbi wa Escape 1 jijini Dar es Salaam

0 comments:

Post a Comment