Pages

Ads 468x60px

Wednesday, April 23, 2014

ZOEZI LA KUTILIANA SAIN YA MKATABA WA UJENZI BUSOKELO NA NHC WAKWAMA

NI BAADA YA MKUU WA MKOA WA MBEYA ABASSI KANDORO KISITISHA KWA KILE KILICHOSEMEKANA KUTOTIMIZA BAADHI YA MAMBO

Add caption
 MKUU WA MKOA AKIBADILISHANA MAWAZO NA WANDISHI WA HABARI KABLA YA MKUTANO NJE YA HOTELI YA HILL VIEW


BAADHI YA WATUMISHI WA SHIRIKA LA NYUMBA WAKIWA KATIKA KIKAO HICHO

                            WAANDISHI WA HABARI WAKISUBILIA MKUTANO KUANZA

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CRISPIN MEELA KUSHOTO WAKIBADILISHANA MAWAZO NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MECKSON MWAKIPUNGA

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MECKSONI MWAKIPUNGA AKIONGEA JAMBO NA KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA MARTIN MDOE
MC WA MKUTANO HUO CHARLES MWAKIPESILE AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA KUONGEA KATIKA MKUTANO

KAIMU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA MARTIN MDOE
MWANYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO MECKSON MWAKIPUNGU AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

MKUU WA MKOA ABASS KANDORO AKIHITIMISHA MKUTANO KWA KUAHILISHA
                                                      HABARI KAMILI


Mkuu wa mkoa wa mbeya ABASS KANDORO amesitisha zoezi la kutiliana saini ya mkataba wa mradi wa ujenzi wa makazi ya watumishi kati ya shirika la nyumba la Taifa na Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe

Akiongea  katika mkutano huo Kandoro amesema watasitsha kwa muda wa wiki moja ili kuweka sawa mambo ambayo  hayakamilika na kufikia kigezo cha kuingia mkataba wa mradi wa ujenzi wa makazi ya watumishi wa Halmashauri hiyo

Hata hivyo amelipongeza sana shirika la nyumba la Taifa kwa kutoa huduma nzuri kwa jamii ya watanzania katika kuwajengea makazi bora na yenye gharama ndogo ili kubaresha maisha yao na kuiendeleza nchi yetu.

 Kwaupande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo MECKSONI MWAKIPUNDA ameishukuru serikali kwa kuipa Halmashauri hiyo kisi cha shilingi milioni miatano kwa lengo la kukamilisha mradi huo, Ambao wanategemea kukamilisha ujenzi wa makazi hayo.

Ameongeza kuwa mradi huo ni endelevu kwani wameliomba shirika hilo kujenga nyumba mia moja za makazi ya kisasa kwa wanachi wa Halmashari hiyo na shirika limekubari kujenga nyumba hamsini kwa awamu ya kwanza.

Nae kaimu mkurugenzi wa Shirika hilo MARTINI  MDOE amesema shirika lina mpango wa kufanya miradi ya kujenga nyumba za garama ndogo kwa wananchi na mpaka sasa miradi hiyo ipo katika Halmashauri kumi na sita nchini ikiwemo Busokelo ambao wanategemea kuwajengea nyumba kumi na nne.

MDOE amewaomba wananchi wa Busokelo kutoa ardhi kwa gharama ndogo ili kupunguza gharama za uuzwaji wa nyumba hizo pia ameitaka Serikali ya mkoa wa mbeya kuondoa urasmu katika kutekeleza miradi hii kwani kati ya mambo yaliyo sababisha kusitishwa kwa kutiliana sahihi ni pamoja na kuwataka kuandika baraua Tamisemi kitu ambacho katika Halamashauri zingine hazifanyi hivyo.

0 comments:

Post a Comment