Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 18, 2014

Kanisa la Moraviani ya zidi kupoteza asili yake,


Ni katika misingi,miongozo na taratibu zake kuiga kutoka  katika madhehebu mengine na kuacha kutunza na kudumisha tamaduni zetu na kuwa enzi  waasisi wa kanisa hilo.


 Kwaya ya vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Nzovwe katika mashindano ya mtaa wa mbeya


  Kwaya ya Vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Mbeya mjini katika mashindano ya Mtaa wa Mbeya


 Kwaya ya Vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Itiji wakiimba katika mtaa wa mbeya 




            Kwaya ya Vijana (A) Kanisa la Moraviani Ushirika wa Mabatini




Kwaya ya Vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Meta wakiwa katika shughuli ya kushindana kaika mashindano ya Mtaa wa Mbeya


Huu ni mtazamo wangu Juu ya Kanisa la MORAVIANI Soma hapo chini

 Na Charles Abraham

Kanisa la Moravian yazidi kupoteza asili yake,

Ni katika misingi,miongozo na taratibu zake kuiga kutoka  katika madhehebu mengine na kuacha kutunza na kudumisha tamaduni zetu na kuwa enzi  waasisi wa kanisa hilo.

Nimekua nikitafakari kwa kina sana juu ya kanisa langu la Moravian Tanzania linaloitwa kanisa la Ndugu. Nikweli sipingani sana na msimamo na msemo huo kwamba ni kanisa la ndugu na ukweli unabakia kua ni kanisa la ndugu.

Kwa nini sipingani na msemo huo, ni kutokana na mfumo wake katika miongozo, taratibu, tamaduni zake na misingi asili. kweli ni ya kiu ndugu najivunia sana kuwa mmoja wa Ndugu, sijawahi jutia na wala sitajutia nina upenda sana Umoraviani wangu

Leo nimejitokeza katika ukurasa huu kutaka kujaribu kuangalia kwa kina na kwa akili zangu ndogo sana lakini kuna vitu navikumbuka katika kumtu mikia Mungu nikiwa katika kipande hiki cha kanisa la Moraviani kabla na baada ya kua muumini  wa imani hii.

Nachelea kusema haya, kwani nakumbuka siku nilipotakiwa kuwa mmoja wa waamini  wa kanisa hili kulikua na taratibu nyingi sana unazozipitia ili kujihakikishia kua mmoja wao wa watu wanaotakiwa kuwa washiriki halali na mwenye sifa na vigezo vya kuitwa huyu ni Mmoraviani mwenzetu.

Nakumbuka sana jinsi mzee wa kanisa alivyo heshimika na waumini wake tofauti na sasa, kwani yeye alikua na dhamana kubwa usipo muheshimu huyu wewe kupata huduma yoyote katika kanisa, usahau mpaka pale mzee wa kanisa akutambue na kukuwasilisha katika vikao harali vya maamuzi.

Najaribu kupitia mambo machache tu kati ya mengi yaliyokua msingi na msimamo wa kanisa lakini kwa sasa yameachwa na kujikuta kanisa la Moraviani linagongana katika baadhi ya mambo, Hebu kumbuka kwamba hapakua na maamuzi yoyote ambayo yaliamuliwa na mtu mmoja na kisha ya kaingia kwenye utekelezaji tofauti na sasa.

Kila jambo lilipitia katika vikao husika na kujadiliwa kwa kina na kisha kulitolea maamuzi ya pamoja na kuingia katika utekelezaji, na hapa mimi nadhani ndipo chimbuko la kauli hii ya Kanisa la ndugu kwamba hakuna alie juu ya mwingine wote sawa sawa, 

Leo hii watu wana msingizia Roho mtakatifu, kutaka kupitisha maamuzi yao utakuta mtu ama mtumishi akisema nime sukumwa na Roho nifanye hivi. Jamani Roho Mtakatifu gani amevunja utaratibu, na kuleta mgawanyiko na  manung`uniko kwa wengine? 

Siku moja nikiwa ndani ya moja ya ibada zetu katika taratibu za kawaida kama wamoraviani walivyo na taratibu za ibaada zao, Ilifika nafasi ya kufanya huduma ya watu walio jitenga kurudi kundini wale waliofuata taratibu za vikao waliitwa mbele kwa lengo la kutubu na kumrejea Mungu wao,

Nika sikia kwa masikio nakuona kwa macho yangu mchungaji akisema leo natoa promoshen kwa kila anaejua alijitenga ama amejitenga na kanisa  apite mbele ili tumrudishe kundini pamoja na hawa waliopita mbele, sikuamini masikio yangu kwamba hivi kanisa letu limefikia hapa kutoa promosheni?

Da! Nilishangaa sana pamoja na hilo siku nyingine nilisikia kiongozi mkubwa wa kanisa aliepewa dhamana ya kuliongoza kwanisa akasi mama mbele akasemea wale wote ambao hawaja okoka pita mbele tuwaongoze sala ya toba He! Hizi tamaduni ni za Moraviani kweli?

Naomba nieleweke siupingi wakovu nami pia nimeokoka, lakini napinga destuli za waokovu zisizo za kibiblia. Najaribu kuangalia tamaduni za Kimoraviani tangu mwanzo lilikuwepo hii? Kama halikuwepo tumelitoa wapi na liko wapi la kwetu? Wakuu wa kanisa hili naomba mnisidie maswali haya.

Ndugu zangu kila lililo kuwepo katika taratibu na tamaduni zetu awali lilikua na makusudi sana, kama tunataka kwenda na wakati tufanye hivyo pasipo kuharibu asili yetu, Ni kweli dunia imekua na utandawazi si kwa Moraviani tu, hata kwa makanisa mengine upo lakini wametunza asili yao.

Nakumbuka mwaka mmoja tukiwa katika maandalizi ya mkutano vijana (b) wa mtaa wa Mbeya mwaka fulani kulitokea ubishani  mkubwa sana ilipofika  agenda ya kumpata mtu wa kuja kukagua mashindano  katika idara ya uimbaji, baadhi ya watu wali pendekeza aje mwalim Chifupa, na dhani jina hili kwa Moraviani sana huku mbeya wanalikumbuka sana.

Swala hili lilipingwa vikali na baadhi ya viongozi katika kulipitisha jina hilo kila mmoja akitoa maoni yake kwamba wame choshwa na ukaguzi wake wengine wakidai alikua akipendelea baadhi ya kwaya kwakua amezifundisha yeye mwenyewe sana kwaya ya vijana uashirika wa mabatini.

Wengi walikubaliana na wazo hilo la kubadilisha waamuzi, na ndipo kikao hicho kilikubaliana kwenda katika chuo cha Kidugala seminali, kilichopo Mkoa Njombe  chuo hiki kina milikiwa na kanisa la Kilutel (KKKT) kwa makubaliano hayo walikuja wakaguzi kutoka huko wakakagua na kutoa matokea lakini haikua dawa yakumaliza ubishanibado lawama za  kupendelewa kwaya fulani ziliibuka tena.

Mwaka uliofuata maandalizi ya uimbaji kwaya nyingi zilikwenda kutafuta waalimu wa nyimbo kutoka makanisa ya Kiluteli, Huo ukawa mwanzo wa kupoteza asili ya uimbaji wa kimoraviani katika kwaya za vijana mpaka leo hii ninapo andika Tahariri hii nina sikitika na kufadhaika sana moyoni.

Nenda katika shirika mbalimbali za hapa mjini kajionee kwaya nyingi zimecha asili uimbaji wake  kama hawajaiga uimbaji wa kasikazini magharibi basi utakuta wanaimba Kiluteli jamani nani katuloga wa Moraviani? Nini kinasukuma kuuchukia utamaduni na asili yetu mbona kuna wengi wanazipenda na kutukubali lakini tunaziacha bila sababu.

Kwanza ni siwe mchoyo wa fadhila kwa waalimu na waimbaji kwa baadhi ya kwaya kuu zilizo nyingi bado hazijaondoka sana katika maudhui ya ki Moraviani napenda kuwapa pongezi sana kwa kulinda U Moraviani wetu nataka kusema hakuna wa kufanana na Moaraviani.

Kuna siku nilipata nafasi ya kuongea na mmoja viongozi wa kanisa letu nilimuuliza mambo mengi kuhusiana na maswali yangu haya, alinipa jibu jepesi sana ambalo mpaka leo najiuliza kanisa lipo kwa ajili ya watu au watu wapo kwa ajili ya kanisa?

“Unajua mtumishi siku hizi hatupendi kuwalazimisha waumini kufata sana sheria ukifuata sana ngumu waumini wata kukimbia wote na kwenda makanisa mengine na kubakia na kanisa tupu, kwa hiyo tunajaribu kulegeza kidogo mashart ili tuendelee kuwa na waumini wetu wasiondoke” mwisho wa kumnukuu

Ewe mtumishi wa mungu unashindwa kusimamia misingi na taratibu za kanisa na kusema kweli ya mungu kwa kuogopa waumini watakukimbia kweli? Hivi ukija kutana na Babu yetu JOHN HUSS utakuja kumjibu upuuzi huo unaonieleza mimi umeujaza katika kicha chako na kuacha kanisa linateketea na kuelekea kusiko julikana? umesahau ulikubali dhamana na kiapa chako mbele za kanisa na Mungu kwamba utalinda na kuheshimu taratibu za kanisa.

Sitaki kuonekana nahukumu ila nataka kutoa maoni yangu kwenu Wachungaji na viongozi wa kanisa la Moraviani mliopo zamu kwa sasa jiandaeni kujibu maswali mbele za Mungu  mlipolifikisha kanisa lake kwani ninayo imani kila mlipandalo mtalitolea hesabu mbele zake.

Nikajaribu kuangalia taratibu za kanisa lingine kama vile Roman catholic lenye taratibu ngumu tangu mwanzo wa kanisa mpaka sasa waumini wake wanazifuata hadi leo bila kujali wala kukimbiwa na waumini wao mpaka leo hii na wanaendelea kujaa kuliko hata sisiwa Moraviani Tunaojiita kanisa la Ndugu.

Ninayo mengi moyoni mwangu juu ya kanisa langu kwani sikukosea kuwa muamini wake naumia kuona mambo yakienda kombo kwani imani yangu ya kuuona ufalme wa mungu nimeiweka Moraviani naogopa nikashindwa ufikia uzima wa milele kwa kusahau majukumu na miongozo yake.
              
 Usikose toleo lijalo,  
Mwisho



2 comments:

  1. Ushauri wangu kwako ni huu jitazame sana wewe kuliki kutazama watu wanafanya nini kwenye taratibu za kanisa lako pia kumbuka kuwa hutakwenda mbinguni kwa tiketi ya kuwa moraviani kitakacho kupeleka mbinguni ni wakovu wako tu. Hivyo mambo ya taratibu za kikanisa nadhani sio njia ya wewe kwenda mbinguni.kinachotakiwa ni wewe kuyafahamu maandiko ya mungu wako tu.

    ReplyDelete
  2. Article nzuri sana ila bahati mbaya umetumia zaidi MAZOEA kama ndio MSINGI wa kanisa. Misingi ya kanisa Moravian bado ipo ila mazoea ndio ambayo hubadilika kulingana na nyakati, na Wamoravian tuna slogan yetu inayosema

    In Essentials Unity, In non Essentials Liberty, All things in Love.

    ReplyDelete