Ni katika
misingi,miongozo na taratibu zake kuiga kutoka katika madhehebu mengine na kuacha kutunza na
kudumisha tamaduni zetu na kuwa enzi waasisi wa kanisa hilo.
Kwaya ya vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Nzovwe katika mashindano ya mtaa wa mbeya
Kwaya ya Vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Mbeya mjini katika mashindano ya Mtaa wa Mbeya
Kwaya ya Vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Itiji wakiimba katika mtaa wa mbeya
Kwaya ya Vijana (A) Kanisa la Moraviani Ushirika wa Mabatini
Kwaya ya Vijana (A) kanisa la Moraviani ushirika wa Meta wakiwa katika shughuli ya kushindana kaika mashindano ya Mtaa wa Mbeya
Huu ni mtazamo wangu Juu ya Kanisa la MORAVIANI Soma hapo chini
Na Charles Abraham
Kanisa la Moravian yazidi kupoteza asili yake,
Ni katika misingi,miongozo na
taratibu zake kuiga kutoka katika
madhehebu mengine na kuacha kutunza na kudumisha tamaduni zetu na kuwa enzi waasisi wa kanisa hilo.
Nimekua
nikitafakari kwa kina sana juu ya kanisa langu la Moravian Tanzania linaloitwa kanisa la Ndugu. Nikweli sipingani sana na msimamo na msemo huo kwamba ni
kanisa la ndugu na ukweli unabakia kua ni kanisa la ndugu.
Kwa nini
sipingani na msemo huo, ni kutokana na mfumo wake katika miongozo, taratibu,
tamaduni zake na misingi asili. kweli ni ya kiu ndugu najivunia sana kuwa mmoja wa Ndugu, sijawahi jutia na wala sitajutia nina upenda sana Umoraviani wangu
Leo
nimejitokeza katika ukurasa huu kutaka kujaribu kuangalia kwa kina na kwa akili
zangu ndogo sana lakini kuna vitu navikumbuka katika kumtu mikia Mungu nikiwa
katika kipande hiki cha kanisa la Moraviani kabla na baada ya kua muumini wa imani hii.
Nachelea
kusema haya, kwani nakumbuka siku nilipotakiwa kuwa mmoja wa waamini wa kanisa hili kulikua na taratibu nyingi
sana unazozipitia ili kujihakikishia kua mmoja wao wa watu wanaotakiwa kuwa
washiriki halali na mwenye sifa na vigezo vya kuitwa huyu ni Mmoraviani
mwenzetu.
Nakumbuka
sana jinsi mzee wa kanisa alivyo heshimika na waumini wake tofauti na sasa,
kwani yeye alikua na dhamana kubwa usipo muheshimu huyu wewe kupata huduma
yoyote katika kanisa, usahau mpaka pale mzee wa kanisa akutambue na kukuwasilisha
katika vikao harali vya maamuzi.
Najaribu
kupitia mambo machache tu kati ya mengi yaliyokua msingi na msimamo wa
kanisa lakini kwa sasa yameachwa na kujikuta kanisa la Moraviani linagongana
katika baadhi ya mambo, Hebu kumbuka kwamba hapakua na maamuzi yoyote ambayo
yaliamuliwa na mtu mmoja na kisha ya kaingia kwenye utekelezaji tofauti na sasa.
Kila jambo lilipitia katika vikao husika na kujadiliwa kwa kina na kisha kulitolea maamuzi ya pamoja na kuingia katika utekelezaji, na hapa mimi nadhani ndipo chimbuko la kauli hii ya Kanisa la ndugu kwamba hakuna alie juu ya mwingine wote sawa sawa,
Leo hii watu wana msingizia Roho mtakatifu, kutaka kupitisha maamuzi yao utakuta mtu ama mtumishi akisema nime sukumwa na Roho nifanye hivi. Jamani Roho Mtakatifu gani amevunja utaratibu, na kuleta mgawanyiko na manung`uniko kwa wengine?
Kila jambo lilipitia katika vikao husika na kujadiliwa kwa kina na kisha kulitolea maamuzi ya pamoja na kuingia katika utekelezaji, na hapa mimi nadhani ndipo chimbuko la kauli hii ya Kanisa la ndugu kwamba hakuna alie juu ya mwingine wote sawa sawa,
Leo hii watu wana msingizia Roho mtakatifu, kutaka kupitisha maamuzi yao utakuta mtu ama mtumishi akisema nime sukumwa na Roho nifanye hivi. Jamani Roho Mtakatifu gani amevunja utaratibu, na kuleta mgawanyiko na manung`uniko kwa wengine?
Siku moja nikiwa
ndani ya moja ya ibada zetu katika taratibu za kawaida kama wamoraviani walivyo
na taratibu za ibaada zao, Ilifika nafasi ya kufanya huduma ya watu walio jitenga
kurudi kundini wale waliofuata taratibu za vikao waliitwa mbele kwa lengo la
kutubu na kumrejea Mungu wao,
Nika sikia
kwa masikio nakuona kwa macho yangu mchungaji akisema leo natoa promoshen kwa kila
anaejua alijitenga ama amejitenga na kanisa apite mbele ili tumrudishe kundini pamoja na
hawa waliopita mbele, sikuamini masikio yangu kwamba hivi kanisa letu limefikia
hapa kutoa promosheni?
Da!
Nilishangaa sana pamoja na hilo siku nyingine nilisikia kiongozi mkubwa wa
kanisa aliepewa dhamana ya kuliongoza kwanisa akasi mama mbele akasemea wale
wote ambao hawaja okoka pita mbele tuwaongoze sala ya toba He! Hizi tamaduni ni
za Moraviani kweli?
Naomba
nieleweke siupingi wakovu nami pia nimeokoka, lakini napinga destuli za waokovu zisizo za kibiblia. Najaribu kuangalia tamaduni za
Kimoraviani tangu mwanzo lilikuwepo hii? Kama halikuwepo tumelitoa wapi na liko
wapi la kwetu? Wakuu wa kanisa hili naomba mnisidie maswali haya.
Ndugu zangu
kila lililo kuwepo katika taratibu na tamaduni zetu awali lilikua na makusudi sana,
kama tunataka kwenda na wakati tufanye hivyo pasipo kuharibu asili yetu, Ni
kweli dunia imekua na utandawazi si kwa Moraviani tu, hata kwa makanisa mengine upo
lakini wametunza asili yao.
Nakumbuka mwaka
mmoja tukiwa katika maandalizi ya mkutano vijana (b) wa mtaa wa Mbeya mwaka fulani kulitokea
ubishani mkubwa sana ilipofika agenda ya kumpata mtu wa kuja kukagua
mashindano katika idara ya uimbaji, baadhi
ya watu wali pendekeza aje mwalim Chifupa, na dhani jina hili kwa Moraviani sana
huku mbeya wanalikumbuka sana.
Swala hili
lilipingwa vikali na baadhi ya viongozi katika kulipitisha jina hilo kila mmoja
akitoa maoni yake kwamba wame choshwa na ukaguzi wake wengine wakidai alikua
akipendelea baadhi ya kwaya kwakua amezifundisha yeye mwenyewe sana kwaya ya
vijana uashirika wa mabatini.
Wengi
walikubaliana na wazo hilo la kubadilisha waamuzi, na ndipo kikao hicho
kilikubaliana kwenda katika chuo cha Kidugala seminali, kilichopo Mkoa Njombe chuo hiki kina milikiwa na kanisa la Kilutel (KKKT)
kwa makubaliano hayo walikuja wakaguzi kutoka huko wakakagua na kutoa matokea
lakini haikua dawa yakumaliza ubishanibado lawama za kupendelewa kwaya fulani ziliibuka tena.
Mwaka
uliofuata maandalizi ya uimbaji kwaya nyingi zilikwenda kutafuta waalimu wa
nyimbo kutoka makanisa ya Kiluteli, Huo ukawa mwanzo wa kupoteza asili ya
uimbaji wa kimoraviani katika kwaya za vijana mpaka leo hii ninapo andika
Tahariri hii nina sikitika na kufadhaika sana moyoni.
Nenda katika
shirika mbalimbali za hapa mjini kajionee kwaya nyingi zimecha asili uimbaji wake
kama hawajaiga uimbaji wa kasikazini magharibi
basi utakuta wanaimba Kiluteli jamani nani katuloga wa Moraviani? Nini kinasukuma
kuuchukia utamaduni na asili yetu mbona kuna wengi wanazipenda na kutukubali lakini
tunaziacha bila sababu.
Kwanza ni siwe mchoyo wa fadhila kwa waalimu na waimbaji kwa baadhi ya kwaya kuu zilizo nyingi bado hazijaondoka sana katika maudhui ya ki Moraviani napenda kuwapa pongezi sana kwa kulinda U Moraviani wetu nataka kusema hakuna wa kufanana na Moaraviani.
Kuna siku
nilipata nafasi ya kuongea na mmoja viongozi wa kanisa letu nilimuuliza mambo
mengi kuhusiana na maswali yangu haya, alinipa jibu jepesi sana ambalo mpaka
leo najiuliza kanisa lipo kwa ajili ya watu au watu wapo kwa ajili ya kanisa?
“Unajua
mtumishi siku hizi hatupendi kuwalazimisha waumini kufata sana sheria ukifuata
sana ngumu waumini wata kukimbia wote na kwenda makanisa mengine na kubakia na
kanisa tupu, kwa hiyo tunajaribu kulegeza kidogo mashart ili tuendelee kuwa na
waumini wetu wasiondoke” mwisho wa kumnukuu
Ewe mtumishi
wa mungu unashindwa kusimamia misingi na taratibu za kanisa na kusema kweli ya
mungu kwa kuogopa waumini watakukimbia kweli? Hivi ukija kutana na Babu yetu JOHN
HUSS utakuja kumjibu upuuzi huo unaonieleza mimi umeujaza katika kicha chako na
kuacha kanisa linateketea na kuelekea kusiko julikana? umesahau ulikubali dhamana
na kiapa chako mbele za kanisa na Mungu kwamba utalinda na kuheshimu taratibu
za kanisa.
Sitaki kuonekana
nahukumu ila nataka kutoa maoni yangu kwenu Wachungaji na viongozi wa kanisa la
Moraviani mliopo zamu kwa sasa jiandaeni kujibu maswali mbele za Mungu mlipolifikisha kanisa lake kwani ninayo imani
kila mlipandalo mtalitolea hesabu mbele zake.
Nikajaribu
kuangalia taratibu za kanisa lingine kama vile Roman catholic lenye taratibu
ngumu tangu mwanzo wa kanisa mpaka sasa waumini wake wanazifuata hadi leo bila
kujali wala kukimbiwa na waumini wao mpaka leo hii na wanaendelea kujaa kuliko
hata sisiwa Moraviani Tunaojiita kanisa la Ndugu.
Ninayo mengi
moyoni mwangu juu ya kanisa langu kwani sikukosea kuwa muamini wake naumia
kuona mambo yakienda kombo kwani imani yangu ya kuuona ufalme wa mungu
nimeiweka Moraviani naogopa nikashindwa ufikia uzima wa milele kwa kusahau
majukumu na miongozo yake.
Usikose toleo lijalo,
Mwisho
Ushauri wangu kwako ni huu jitazame sana wewe kuliki kutazama watu wanafanya nini kwenye taratibu za kanisa lako pia kumbuka kuwa hutakwenda mbinguni kwa tiketi ya kuwa moraviani kitakacho kupeleka mbinguni ni wakovu wako tu. Hivyo mambo ya taratibu za kikanisa nadhani sio njia ya wewe kwenda mbinguni.kinachotakiwa ni wewe kuyafahamu maandiko ya mungu wako tu.
ReplyDeleteArticle nzuri sana ila bahati mbaya umetumia zaidi MAZOEA kama ndio MSINGI wa kanisa. Misingi ya kanisa Moravian bado ipo ila mazoea ndio ambayo hubadilika kulingana na nyakati, na Wamoravian tuna slogan yetu inayosema
ReplyDeleteIn Essentials Unity, In non Essentials Liberty, All things in Love.