Mzee Isakwisa Mwambulukutu mwenyekiti wa wazee wa chama cha mapinduzi (ccm) akiongea na waandishi wa habari
wazee wa ccm wakisikiliza kwa makini hotuba ya mwenyekiti kwa waandishi wa habari wakitoa tamko lao
Habari kamili
Serikali imeshauliwa
kuwashughulikia wale wote wanao wakashifu waasisi wa Nchi hii.
Mwambulukutu
amesema hayo alipokua akitoa tamko kwa niaba
ya wanachama na wazee wa ccm juu ya kauli mbalimbali zinatolewa katika bunge za
kuwakashifu waasisis wa Taifa hili ambao wamekua ndiyo chimbuko la Nchi yetu
“Sisi kama
wananchama na wazee wa ccm wa mkoa wa mbeya tunapenda kukemea vikali na kwa
nguvu zetu zote na kulaani kauli mbaya zinazotolewa na baadhi ya vijana wetu
katika bunge maalum la katiba kwa kuwakafshifu na kuwakejeli waasisi wetu J. k.
Nyerere na Amani Karume kwakuwa hao ndiyo chimbuko la Taifa hili” Amesema
mwambulukutu
Ameongeza
kuwa kama wanataka kuendelea na Bunge hilo
wanapaswa kuwacha mara moja Lugha hizo za kejeli na kashfa na wajue uhuru wanao utumia unakikomo na kwamba watanzania wote si wajinga na wanapenda
kusikiliza lugha zao wanazotumia.
Pamoja na
hayo wazee hao wamempongeza Rais na mwenyekiti wa chama
hicho J. K Kikwete kwa busara zake na kuruhusu mchakato wa kuunda katiba mpya
ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na pia kwa uvumilivu wake katika kuona
wanakamilisha jambo hili.
Pia wazee
hao wanaunga mkono mfumo wa Serikali
mbili wala si vinginevyo na hawapo tayari kuwasaliti wasisi wa nchi hii isipokua
zifanyike juhudi za ziada katika kuondoa kasoro ndogo ndogo zilizopo ndani ya
muungano.






0 comments:
Post a Comment