Hayo yamebainishwa leo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii katika
semina ya siku nne iliyoandaliwa na kanisa hilo inayofanyika katika ofisi za kanisa hilo zilizopo
Jakaranda jijini Mbeya.
Askofu Alinikisa Cheyo(picha na maktaba yetu) |
Amesema swala
la uwajibikaji kwa watendaji wa kanisa limekua tatizo kubwa ambalo limepelekea kuwepo
kwa semina za mara kwa mara kwa wakuu hao ili kuwajengea uwezo katika utendaji wa kazi zao za kila siku.
“Watumishi wengi wamekuwa wakichaguliwa na Halmashauri kuu ya kanisa bila kujua wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao mara nyingi hujikuta wanafanya kazi wakisukumwa na roho mtakatifu tofauti na viongozi wanaotoka Serikalini hufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko hawa” amesema Askofu Cheyo
Nae Zacharia
Sichone Makamu mwenyekiti wa kanisa hilo amesema wameamua kuendesha semina hiyo
ili kuwajengea uwezo viongozi hao kwa lengo la kuwaimarisha na kuona wanajua
wajibu wao ili wakishindwa kutekeleza majukumu yao basi wajihukumu wao wenyewa kukushindwa
kutekeleza kinacho wapasa kufanya.
“Tunaweza
kulaumiana na kwa makosa mbalimbali kwa wakati mwingine si kwa makosa ya watu
kumbe nikutokana na uelewa mdogo walio nao hawajui wajibu wao, Kupitia mafunzo
haya kila mmoja atajua kinacho mpasa kufanya na kisha kufikia malengo makubwa
na kuleta maendeleo katika kanisa letu” Amesema Sichone.
Kwa upande
wake Agripa Senka mkurugenzi wa uchumi, mipango na maendeleo amesema kumekuwepo
na mpango wa miaka minne ya kuendesha mafunzo ya namna hiyo kwa
hivyo kwani viongozi wengi huchaguliwa bila kuwa na maarifa ya uongozi
kupitia semina hizo zitafanya viongozi kuwa na uwezo wa kiutendaji na kujiamini
katika kazi zao.
Pia Nyandu
Kajange katibu wa wilaya ya chunya ambae ni mmoja wa washiriki wa semina hiyo
amesema wamejifunza kusimama vizuri katika nafasi zao nakupanga mipango ya kazi nyenye utekelezaji mzuri na kujiamini katika uongozi na kuleta maendelao katika
taasisi husika.
mwisho
Katibu mkuu wa kanisa la moraviani Tanzania mmoja wa wakufunzi wa semina akiongea jambo wa wanasemina
Viongozi na wakuu wa taasisi za kanisa la moraviani Tanzania jimbo la kusini magharibi wakisikiliz za kwa makini mafunzo yanayoendelea
Makamu wa mwenyekiti Zacharia Sichone akijangia moja ya mada katika Semina hiyo
Devule mwambije mkaguzi wa ndani wa kanisa akongea kitu katika semina
Mwisho
0 comments:
Post a Comment