Mamlaka Imeahidi kuijenga chemba hiyo
haraka iwezekanavyo ili kuwapunguzia wakazi wa kata ya majengo kero hiyo ndani
ya wiki mbili zijazo ili kulinda afya zao dhidi ya magonjwa ya milipuko.
Baada ya
kilio cha muda mrefu sasa kwa wakazi wa jiji la Mbeya kata ya majengo kwa kile
walichodai kero ya chemba ya majitaka kutililisha maji hayo katika mto wao
unaotumika na idadi kubwa ya wakazi hao kwa shughuli mbalimbali za kijamii na
kuhatarisha afya zao na kuahidi kuijenga chemba hiyo ndani ya wiki mbili.
Akiongea na Mwandishi
wa habari hii ofisini kwake mkurugenzi mtendji wa mamlaka ya majisafi na
majitaka Eng: Simion Shauri amesema hakuwa na taarifa ya tatizo hilo hivyo
amewataka wakazi hao kuwa na subira kwani suala hilo litashughulikiwa haraka
iwezekanavyo.
“Nawaomba
wakazi wa majengo kuwa wavumilivu kwa tatizo walilonalo litatuliwa ndani ya
wiki mbili zijazo na kuwafanya waishi kwa amani kama kawaida, ni kweli sikuwa
na taarifa ya tatizo hilo la sivyo lingekua tayari limetatuliwa kwa muda
muafaka na kuiondoa kero hiyo kwa wakazi ambao wamekua wakilalamika”amesema
Shauri.
Ameongeza
kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Mbeya kujitokeza kwa wingi ili kujiunga na
huduma ya mtandao wa uondoshwaji wa majitaka kutoka katika majengo yao na kwa
sasa mamlaka imeondoa gharama za kuunganishwa katika mtandao huo na kuwapa
mabomba mita 30 bure wateja wake ili kuhamasisha na kuwapa unafuu wa huduma
hiyo.
Naye Eng:
Mloelya Paul amesema tatizo hilo lilisababishwa na ujenzi wa barabara uliokuwa
ukifanywa na Halmashauri ya jiji la Mbeya na kubomoa chemba hiyo na kuziba na
hivyo kufanya shughili ya kuizibua kuwa ngumu kwa kua ilizibwa na mawe makubwa
ambayo yanatakiwa kuchimbwa ili kuyatoa.
Eng: Mloelya Paul akisoma Risala kwa mgeni rasmi |
“tatizo hilo lipo kwa muda mrefu sasa tulikuwatunashughulikia
bajeti yake ambayo mpaka sasa imekamilika ndani ya wiki hii tutaanza
kulichughulikia na ndani ya muda wa wiki mbli zijazo litakua limekamilika
wakazi hao wategemee kuondokana na kelo hiyo iliyosababishwa ujenzi wa barabara
za halmashuri ya jiji ambao hubomoa miuondo mbinu hiyo mwanapoendesha shughuru
zao hizo” amesema Mloelya.
Hatua hiyo
imekuja baada ya kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa kata ya majengo ambao walikumbwa
na mshangao mkubwa baada ya mamlaka hiyo kujenga chemba mpya kwa muda wa masaa
24 na kuizindua katika maadhimisho ya wiki
ya maji na kuicha chembe iliyokua kero kubwa kwao iliyopigiwa kelele kwa muda
mrefu na kutopatiwa ufumbuzi,
Chemba ya majitaka inayotililisha majitaka katika mto Dauseni ambayo ni kero kubwa kwa wakazi wa kata ya majengo
Mto huo maji yake hutumika kwa matumizi mbalimbali kama mwandishi wa habari hii alivyo wakuta wanafunzi wa shule ya Sekondali ya Rejiko wakichota maji hayo yenyekuchanganyikana na majitaka
0 comments:
Post a Comment