Hayo yamejili katika kongamano la wasomi hao lililohusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuonesha nia yao ya kumshawishi kugombea nafasi hiyo.
IDD MAMBO KATIBU ITIKADI NA UENEZI CHUO KIKUU TEKU AKIMKARIBISHA MSEMAJI WA TAMKO HILO.
BAADHI YA WANACHAMA WA CCM NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WALIOKUWEPO KATIKA KUTOA TAMKO HILO
OSCAR MWAIHABI KATIBU WA SHIRIKISHO LA WANAZUONI AKITOA TAMKO KWA NIABA YA WANAZUONI MKOANI MBEYA KWA WAANDISHI WA HABARI
Soma hapa:
Na: Charle Abraham
Sirikisho la vyuo vikuu mkoani Mbeya wamtaka Prof: MARCK MWANDOSYA kujitokeza kuwania uraisi uchaguzi mkuu ujao.
Hayo
yamejili katika kongamano la wasomi hao lililohusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuonesha nia yao ya
kumshawishi kugombea nafasi hiyo
Katika siku za karibuni kumekuwapo mjadala mkubwa ndani ya
CCM juu ya mtu atakayepitishwa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho, na
ilizidi baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa mwanachama ambaye atateuliwa
na CCM kugombea urais hayumo miongoni mwa waliojitokeza na kuwataka wanachama
kuwashawishi watu wenye sifa wajitokeze
Wakati joto la urais
likizidi kupanda ndani ya CCM kutokana na hofu ya baadhi ya majina mazito ya
wagombea wa nafasi hiyo kuendelea kujitokeza na ikiwa ni pamoja na kujinadi kwa
sili hali hiyo imechukua hatua zaidi baada ya shirikisho la vyuo vikuu mkoani
Mbeya kufaya kongomano la uchaguzi mkuu lililofanyika
katika ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini hapa nakuchukua nafasi hiyo ya
kumshawishi Prof: MARCK MWANDOSYA kugombea nafasi ya uraisi.
Akisoma tamko loa wanazuoni hao mbele ya waandishi wa habari
katibu wa shirikisho hilo OSCAR MWAIHABI toka chuo kikuu cha tumaini amesema
wamefikia uwamuzi huo baada ya kuona ndani ya chama hicho hakuna kiongozi
mwenye sifa ya kufanana nae na hivyo wangeona Tanzania ijayo ikiongozwa na
kiongozi huyo.
“Sisi wanazuoni tumeona kuwa wewe Prof: MARK J. MWANDOSYA unafaa kabisa kupokea kijiti cha
uraisi kutoka kwa JAKAYA KIKWETE kwakua unafaa ni tofauti na wengine wote
waliojitokeza kutangaza nia katika Chama Cha mapinduzi kutokana nauongozi ulio
wahi kushiriki kuongoza hujawahi kupata tuhuma yoyote mpaka leo hii, pia Taifa
linahitaji kiongozi mwenye hekima na maamuzi magumu hata utafiti unaonesha
uwezo ulionao wa kiuongozi” amesema Mwaihabi
Ameongeza kua Mwandosya ni mengi mazuri ameyafanya katika
uongozi wake ndani ya Taifa hili, Hivyo wao kama wanazuoni wanamuomba kwa
heshima kubwa ashawishike kugombea nafasi hii adhimu katika Taifa hili ya
Uraisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama Cha mapinduzi kama Dr.
Jakaya Kikwete alivyo wataka wanachama wa CCM kuwashawishi watu wenye uwezo
ambao hawajajitokeza kutangaza nia zao wajitokeze.
Hadi sasa, wanachama waliojitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, January Makamba (Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia), Hamisi Kigwangala, na Lazaro Nyalandu ambaye ni waziri wa Maliasili na Utalii.
Lakini pia wako wanaotajwa kuwania urais lakini hawajatangaza ambao ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sita, William Ngeleja, Emmanuel Nchimbi, Mwigulu Nchemba, Stephen Wasira, Bernard Membe na Edward Lowassa ambaye ameibua mjadala kati ya kambi yake na zinazompinga.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment