Tazama ilivyo anzwa kuchomwa moto |
Tatizo la kujichukulia
Sheria mkononi limeendelea kuwa kubwa kwa jamii ya watanzania, katika sakata la hivi karibuni ambapo baadhi
ya watu walikuvunja na kuichoma moto nyumba ya mkazi mmoja wa mtaa mbwile b jijini
Mbeya kwa tuhuma za kubaka na kumuua mwanafunzi wa miaka nane.
Nyumba ikiwa imebomolewa |
Katika hali
isiyo ya wakawaida wakazi hao wamejikuta wakichukua sheria mkononi kwa kuivunja
na kuichoma moto nyumba ya Mariamu
kasonta baada ya kumtuhumu mlinzi wake kumbaka mwanafunzi wa darasa la
pili katika shule ya msingi majengo mwenye umri wa miaka nane jina
limehifadhiwa na kisha kumkuta akiwa ameuwawa na kutupwa katika shimo la maji
taka.
Wakazi hao
ambao walipimga vibaya mlinzi huyo aliejulikana kwa jina moja la Charles ambae
alikamata siku ya tatu tangu kutokea kwa tukio hilo na kuokolewa na askali
polisi waliowahi kufika katika eneo la tukio, wananchi hao walivamia
nyumba ya bosi wake kisha kuibomoa na
kuchoma moto ambapo kikosi cha zimamoto kilifika na kufaninikiwa kuuzima moto
huo kabla ya kuiteketeza nyumba hiyo kabisa.
Askali wa jeshi la polis baada ya kufanikiwa na kuwadhibiti wananchi kiatika kutekeleza uharifu huo
Mwenyekiti wa mtaa mzee Bukuku akiwataka wakazi wa eneo hilo kuondoka na kuacha kuibomoa nyumba hiyo,
Zunda gabliel kaimu mkuu wa kituo cha polisi kati akiongea na wananchi kufanya ulinzi wa nyumba iliyokua ikibomolewa
Henry kakobe askali wa kata ya Nonde akiwatuliza wananchi katika mkutano ulioitishwa na mwenyekiti wa mtaa huo.
Wananchi waliofika kwenye mkutano wakitaka mtu aliehusika na mauwaji ya mwanafunzi atajwe.
Askali kanzu wakiimalisha ulizi katika mkutano wa wananchi wa Nonde Mbeya
Rebeka mwalyego afisa mtendaji wa mtaa wa mbwile (b) akiongea na waandishi wa habari katika eneo la tukio
0 comments:
Post a Comment