Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima
malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria
Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa
kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka
mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.
.............
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu
amewataka watanzania kwa pamoja kuungana kupambana na ugonjwa wa Malaria
ili kusaidiana na serikali kutokomeza ugonjwa huo ambao husababisha
vifo vya watu wengi nchini.
Waziri
Ummy ameyesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa
ni siku ya Maralia Duniani ambapo huadhimishwa Aprili, 25 ya kila mwaka
na kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu ili kutokomeza ugonjwa huo.
“Msisitizo
mkubwa wa Wizara yangu ni kwa wananchi na wadau wote kuona umuhimu na
kutoa kipaumbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria kwa
kuhakikisha matumizi sahihi ya mikakati iliyopo katika kuuthibiti
ugonjwa huu,
“Iwapo
mikakati hiyo itatekelezwa ipasavyo ni dhahiri kuwa maambukizi
yataendelea kupungua kwa kiasi kikubwa na hatimaye kumaliza kabisa
tatizo hili,” alisema Waziri Ummy.
Kaimu
Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria, Dkt.Renata Mandike
(kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na utekelezaji wa udhibiti wa
Malaria nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo
pichani). Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Ummy Mwalimu.
Baadhi ya wataalam wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu.
Fundi
sanifu maabara, Habiba Malima akimchukua damu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu kwa kipimo cha
malaria Rapid Diagnosist Test(mRDT), kipimo hicho ni cha haraka na
huchukua dakika ishirini kugundua kama una Malaria, kipimo hiki kilianza
kutumika nchini mwaka 2009.
Mwandishi
wa habari na mmiliki wa globu ya mzee wa matukio, Richard Mwaikenda
akichukuliwa kipimo cha malaria na fundi sanifu maabara Habiba Malima
ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani katika ukumbi wa viwanja
vya Bunge.
Afisa habari wa idara ya habari Maelezo, Eleuteri Mangi akipima malaria kwa kipimo cha mRDT.
Mwandishi wa habari kutoka Clouds media, Kijah Yunus akipima Malaria.
0 comments:
Post a Comment