Pages

Ads 468x60px

Monday, May 15, 2017

WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA MBEYA WAWAKUMBUKA WAZEE.Na Charles Mwaipopo.
WAUGUZI wanaofanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wameadhimisha sherehe yao kwa Kutoa msaada kwa Wazee waishio kwenye mazingira magumu.

Wauguzi hao walifanya hivyo katika kuadhimisha Sikukuu ya Wauguzi duniani  ambayo huadhimishwa  Mei 12 kila  mwaka  wakimkumbuka muuguzi aliejulikana kama Night Ngel.

Akizungumza kwa niaba ya Wauguzi wenzie,katika maadhisho hayo JUDIKA PAULO MINJA  amesema wameamua kuadhimisha sherehe hizo kwa kusaidia wazee waishio katika mazingira magumu.

Minja ametoa wito kwa  serikali kuona namna ya kuwasaidia Wazee hao kupata Bima ya afya ili kukabiliana na changamoto za matibabu ya magonjwa mbalimbali.

Nae mratibu Wazee waliotembelewa wanaoishi katika Kituo cha Tumaini la Wazee kilichopo Majengo jijini Mbeya,BONIVENTULA MWALONGO amewashukuru  wauguzi hao kwa moyo walio uonesha na kwamba Taasisi hiyo ipo kuwakusanya Wazee ili kuwasaidia kukabiliana  na changamoto za uzeeni.

Wauguzi hao  wametoa msaada wa chakula ikiwepo  gunia mbili za mchele, Sukari katoni nane pamoja na Sabuni. Vyote vikiwa na thamani ya Tshs 800,000.

0 comments:

Post a Comment