Shirika
la Umeme nchini (Tanesco), limefanikiwa kukarabati mashine namba 6
iliyokuwa imeharibika na kuiwasha kwa ajili ya kutoa huduma ya umeme kwa
mikoa
ya Lindi na Mtwara.
Hatua
ya kuwashwa kwa mtambo huo ni juhudi za shirika hilo za kuimarisha hali
ya upatikanaji umeme kwa wananchi kusini huku ikiwa ni siku moja baada
ya Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani alipotembelea Kituo cha
kufua umeme kwa gesi .
Akizungumza
leo mjini hapa, Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Mhandisi Dk. Tito Mwinuka
ambaye amepiga kambi mkoani humo pamoja na watalaamu wengine, alisema
kuwa mitambo iliyokuwa ikifanya kazi ilikuwa minne lakini baada ya
juhudi kubwa za wataalamu wa Tanesco hadi kufikia jana jioni
wamefanikiwa kuwasha mashine hizo zenye uwezo wa kuzalisha Megawati 16.
“Tanesco
tumeshagiza vipuri vya aina mbalimbali ili kutengeneza mashine hizi na
pia Shirika katika kuhakikisha kazi inakwenda kwa kasi zaidi itaongeza
nguvu ya wataalamu kutoka vituo vingine vya TANESCO hapa nchini.
“Tunawaomba
wateja wetu wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kuwa wavumilivu
wakati uongozi wa Shirika, Kanda na Mkoa ukiendelea na juhudi za
kumaliza kabisa upungufu wa umeme katika mikoa hii,” alisema Dk.
Mwinuka.
Alisema
kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya umeme kwa mikoa hiyo, alisema
Shirika limeshaanza taratibu za kupata Megawati nne za haraka kwa
kuagiza mitambo mwili mipya.
“Tuna
imani kubwa na wafanyakazi wa Kituo cha kufua umeme wa gesi cha Mtwara
na wataweza kukarabati mitambo yote pindi vipuri vitakapowasili,”
alisema
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji huyo amewashukuru wananchi wa mikoa ya Lindi na
Mtwara kwa uvumilivu waliouonesha katika kipindi cha matengenezo ya
mitambo hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Tito Mwinuka, (wakwanza
kushoto), na viongozi wengine wa Shirika hilo, wakifuatilia maendeleo ya
ukarabati wa mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara leo Oktoba 17, 2017.
0 comments:
Post a Comment