WATANZANIA wametakiwa kuwa na
utaratibu wa Kukatia Bima Mali zao ili kujikinga na hasara pindi majanga
mbalimbali yanapotokea na kupelekea vilio kwa Wahanga.
Wito huo ulitolewa hivi
karibuni na Kamishna wa Bima nchini Dk. Baghayo
Saqware alipokuwa akizungumza na mtandao huu kuhusu mwitikio wa
Watanzania katika kukata Bima za Mali zao alipokuwa akihani msiba wa Baba mzazi
wa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini, Elia Kajiba Marehemu
Paul Kajiba.
Kamishna huyo alisema kuwa na
Bima kunamuondolea hofu ya kupoteza Mali kutokana na kuwa na uhakika wa kuweza
kulipwa fidia na Kampuni ya Bima baada ya aidha kupata ajali ya Moto,tetemeko
la ardhi au kimbunga kinachoweza kusambaratisha Mali pamoja na mafuriko.
Alitolea mfano Wahanga wa Soko
la Sido jijini Mbeya ambao walikumbwa na janga la Moto lililopelekea kuteketeza
Mali na bidhaa mbalimbali zilizokuwemo kwenye maduka yao lakini waliokuwa na
Bima waliweza kulipwa na hatimaye kupata mitaji ya biashara zao.
Aliongeza kuwa kuna aina nyingi
za Bima ambazo kila Mtu anaweza kukata ikiwemo Bima ya Mali, ajali, Maisha na
Bima ya Afya kwa ajili ya kuwezesha familia kupata matibabu muda wowote
wanapougua.
Hata hivyo akitoa salam za
rambi rambi katika ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Moravian
Usharika wa Mjini jijini Mbeya na kuzikwa katika makaburi ya Nonde, Kamishna
huyo aliwataka jamii kuishi kwa upendo na kufuata matendo mema ya Marehem.
Naye Meneja wa Bima Kanda ya
Nyanda za juu kusini, Consolata Gabone alisema upendona mshkamano mahala pa
kazi ni ishara ya ushirikiano ambao umeoneshwa na kuguswa na Kamishna hadi
kuhudhuria ibada ya mazishi.
“Sio Kawaida kwa Kamishna kuja
huku mkoani kushiriki msiba wa kufiwa kwa mfanyakazi wake kwani alikuwa na uwezo
wa kutuma mwakilishi hivyo tunajifunza kuishi kwa upendo na mshikamano sehemu
zetu za kazi” alisema Gabone.
Meneja wa Bima Kanda ya
Nyanda za juu kusini, Consolata Gabone menye brauzi ya kijivu akishiriki ibaada ya mazishiMkurugenzi wa Ukaguzi wa Bima Nyanda za juu kusini, Elia Kajiba mtoto wa marehemu akitoa heshima zake za mwesho
Ndugu, Jamaa na marafiki wakiwa ndani ya ibaada ya mziashi iliyofanyika katika kanisa la Moraviani Mbeya mjini
Msafara wa magari kuelekea makaburi ya Nonde kwa mazishi
Mchungaji wa kanisa la moravia Osia Mbotwa akiongea jambo makaburini
Jeneza lilili chukua mwili wa marehemu Paulo kajiba likishushwa kaburini
0 comments:
Post a Comment